Bunge la 11 mkutano wa pili kikao cha kwanza la Jamhuri ya
muungano wa Tanzania limeanza leo mjini Dodoma ambapo limefunguliwa kwa
dua
pamoja na kula kiapo cha uaminifu kwa wabunge 11, ambao wamechaguliwa na
wengine kuteuliwa na Rais baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge.
Wabunge hao
ni pamoja na Goodluck Mlinga wa Jimbo la Ulanga, Shaaban Shekilindi wa Lushoto,
Godbless Lema wa Arusha Mjini, Omar Kigoda Jimbo la Handeni, Deogratias Ngalawa
wa Ludewa na Rashid Chauchau wa Masasi.
Spika wa Bunge la Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania..Mh. Job Ndugai |
Maswali
kadhaa yameulizwa na wabunge na kisha kujibiwa ambapo kwa siku ya leo jumla ya
maswali ya msingi ya kawaida 125 yanategemewa kuulizwa na kujibiwa.
Maswali
yaliyoonesha kuwagusa wengi ni pamoja na maswali yaliyohusu tatizo la njaa
linalokabili maeneo mbalimbali hapa nchini, elimu, maliasili pamoja na maji.
Kuhusu tatizo la njaa serikali imesema itaendelea kufanya
tathmini ya hali ya njaa nchini na kwamba hakuna mtanzania yeyote atakayekufa
njaa kutokana na ukosefu wa chakula.
Akijibu swali la Mbunge wa Mpwapwa mkoani Dodoma George
Malima Lubeleje aliyetaka kufahamu hatua ambayo serikali imechukua kukabilina
na njaa katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu amesema serikali imeanzaa kugawanya
chakula cha msaada.
No comments:
Post a Comment