Monday, April 13, 2015

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 12/APRIL/2015

Maelfu ya watu wamekusanyika katika Chuo Kikuu Cha Manabii kwenye ibada ya jiji iliyofanyika Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha na
kupokea matamko ya Kinabii pamoja na kufunguliwa vifungo mbalimbali.
Katika ibada hiyo Nabii mkuu mheshimiwa Dr GeorDavie amewaondolea hofu watu wanaoamini nguvu ya kinabii nakutamka kuwa mienzi nane iliyobaki ili kumaliza mwaka huu Mungu atawapa wepesi katika kazi  idara zote za usalama katika nchi ya Tanzania na kila kitu chochote kibaya kilichojificha popote kitaonekana kwa urahisi.
Kwa upande wa Balozi  wa Nabii MKuu  Apostle Sekela Amesema kuwa mahali popote anapokuwepo nabii watu wanaomwamini ni lazima kunyenyekea zaidi na kuwa watii ili roho ya Nabii na nguvu zake iwe maishani mwao kwa ajili ya mafanikio mbalimbali.
Aidha katika  ibada hiyo watu wamefunguliwa katika  vifungo mbalimbali  ikiwemo  wale waliokuwa wakiteswa na magonjwa kama kupooza,kifafa na nguvu za giza ambapo nabii mkuu Dr. GeorDavie amewatamkia watu wote wanaomuamini nabii katika wiki hii kwamba Kabla maadui zao hawajazinduka Mungu amewatekea nyara watu hao na wamepokea ulinzi kutoka katika serikali ya ufalme wa Mungu.
                                   SIKILIZA NA DOWNLOAD NENO LA KUNABII LA WIKI.



SIKILIZA NA DOWNLOAD NENO LA UNABII WA MIEZI MI NANE(8) KWA VYOMBO VYA USALAMA VYA TANZANIA.

No comments:

Post a Comment