Maelfu ya watu waliokusanyika katika chuo
kikuu cha Manabii Kisongo katika ibada ya jiji wamepokea Baraka mbalimbali za kinabii
na kufunguliwa katika vifungo mbalimbali.
Katika ibada hiyo Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr.GeorDavie ametamka Baraka kwa watu wote wanaomwami Nabii kupokea siku saba za ukamilifu wa uponyaji katika miili yao huku wakiendelea na siku 41 za maadui kubeba mizigo yao.
DR.
GeorDavie ametangaza kuwa mienzi tisa hii iliyobaki ili kumaliza mwaka
wa 2015 ni mienzi ya kuona faida katika kila eneo na pia ametamka kwa watu
wanaomuaminia nabii kuzaa matunda kila mwezi katika kila eneo.
Amefafanua kuwa maneno ya kinabii yanayotamkwa
kila siku ni ya thamani hivyo ni lazima
yafanyiwe kazi kwani wapo maelfu ya watu wanaotamani kuwa na neema ya kuwa na nabii
katika nchi zao.
Hata hivyo mtumishi mwanafunzi William
James ameitaka jamii kutambua wakati na mambo ya kimungu
yanavyoendelea na kumsikiliza mungu anayezungumza sasa kwa wakati wetu na siyo
kusismamia mambo yale Mungu aliyoyafanya na watu wa zamani.
Sanjari na hayo watu wengi wameweza
kufunguliwa vifungo mbalimbali ikiwemo watu waliokuwa kukosa raha na amani
wametamkiwa furaha na amani na hali hiyo kutoweshwa kwao,huku nabii mkuu
akitamka kwamba katika wiki hii tutakumbuka mahali ambapo Mungu ametutoa na
sasa tulipofika.
No comments:
Post a Comment