Tukiendelea kukumbuka tamko la Unabii kutoka kwa Nabii Mkuu Dkt. GeorDavie kuhusu majanga mbalimbali nchini,takribani watu watano wamejeruhiwa ,
katika ajali iliyohusisha magari mawili ikiwemo lori la Mizigo Semitrela na basi la abiria likitokea Arusha
kuelekea Dodoma .
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi katika eneo la Kisongo uwanja wa
ndege(Arusha Air Port) ambapo ajali hiyo
imehusisha basi la kampuni ya Arusha Express lenye namba T 206 BEF na lori la
mizigo kampuni Crewary lenye namba T 493 AED.
Kwa mujibu wa majeruhi na shuhuda watukio hilo chanzo cha ajali hiyo
ni dereva wa basi lilokuwa likitokea Arusha kuelekea Dodoma alipotaka kupita
gari lingine lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na hamadi alikutana
na lori la mizigo lililokuwa linatokea Manyara.
Kufutia ajali hiyo baadhi ya wakazi
wa jiji la arusha wamelitaka jeshi la polisi kufanya ukaguzi mara kwa mara ili
kubaini baadhi ya watu wanaondesha vyombo vya usafiri wakati huo wakiwa hawana
sifa za kuendesha magari.
Kwa upande Bwana Miraji Ally mkazi wa Arusha amesema
kumeibuka wimbi la madereva wanaondesha magari hasa ya abiria wakati huo wakiwa
wanafanya mashindano wao kwa wao hali inayosababisha kutokea ajalia ambazo zimekuwa zikigharibu
maisha ya watu kila siku.
Aidha kamanda wa jeshi la Polis Mkoa
Wa Arusha Leberatus Sabasi amethibitisha
kutokea kwa ajli hiyo na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea
kufanyika huku majeruhi wakiendelea
kupatiwa matibabu katika hospital ya Mkoa Maunt Meru.
No comments:
Post a Comment