Friday, March 6, 2015

MWAKA 2015 WAANZA KUNG’ATA WAGANGA WA KIENYEJI KAGERA.



Ikiwa ni baada ya tamko la Kinabii juu ya mwaka 2015 kuwa ni mwaka wenye meno na unang’ata kwa waganga wa kienyeji,washirikina na wachawi.Hatimaye
 JESHI la Polis mkoani Kagera limeanza opereisheni ya kuwasaka waganga na wapiga ramli,ikiwa ni harakati za kutokomeza vitendo vya mauaji vinavyodaiwa kusababishwa na baadhi ya waganga wa kienyeji kwa kutoa ushauri kwa waharifu.

Opereisheni hiyo endelevu imeanza  Machi 4 kwa kuwahusisha katika wilaya ya Biharamulo kwa kuwashirikisha askari Polis pamoja na kikosi cha Mali Asili,nakufanikiwa kuwakamata jumla ya wapiga ramli 18 waliokuwa katika viji vya kata nne za Kabindi,Nyamigogo,Runazi na Nyabizozi zote zikiwa ndani ya tarafa Nyarubunga wilayani Biharamulo.

Kamanda wa jeshi la Polis mkoani hapa Hennry Mwaibambe,akiongea katika tukio hilo katika kituo cha Polis Kabindi,Opereisheni hiyo imeanza ili kuhakikisha vitendo vya mauaji na kishirikina vinatokomezwa,kwani vitendo vya mauaji vimekuwa vikishamiri katika maeneo ya wilaya ya Biharamulo.

Kamanda Mwaibambe alisititiza kuwa opereisheni hiyo si nguvu ya soda,bali itakuwa endelevu kwani wapo baadhi ya wahusika na vitendo vya uharifu wa mauaji wamekuwa wakihusika katika mauaji ya binadamu kwa kutafuta viungo vya binadamu hasa kwa kuwaua binadamu wenye ulemavu wa ngozi(Albino) hivyo jeshi la Polis mkoani Kagera kwa kushirikiana na maafisa wanyama poli poli la  Burigi,watahakikisha wanapambana na hali hiyo.

"Jeshi letu limejipanga kuhakikisha linalinda watu hawa(wenye ulemavu wa ngozi)tunaomba jamii iwe tayari kuwafichua wale wote wenye dhamira na kujihusisha katika vitendo hivyo vya kijama,vitendo hivi vinalitia doa taifa letu,lazima tuhakikishe tunatokomeza hali hii!natoa onyo kwa wale wanajihusisha na shughuli ya upigaji ramli na uganga wa kienyeji.tabia hii haivumiliki tena!"alisisitiza Kamanda Mwaibambe.

Aliongeza mara baada ya kukamilika taratibu za mahojiano,watuhumiwa wote 18 waliokamatwa watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yaliyo mbele yao.
                                                                                                                        Chanzo ITV