Serikali
Imesema tatizo la ukuajiwa uchumi usioenda na maisha halisi ya mtanzani
umechangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kasi kubwa ya
ongezeko la watu na
kilimo duni.
Hayo
yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na waziri wa fedha na mipango Dr.Philip
Mpango wakati akizungumzia mkakati wa taifa wa
maendeleo endelevu katika mwaka wa fedha 2015-2017.
Dr. mpango
amesema ili kuhakikisha uchumi unakua ni vyema mfumo wa utumiaji fedha za nje
urekebishwa ili kuendana na tangazo la serikali mwaka 2007 lililokuwa
linaelekeza malipo yote yalipwe kwa mfumo wa shilingi kwani ufumo uliopo sasa umekuwa ni changamoto
katika ukuaji wa uchumi hapa nchini.
Hata hivyo mpango amesema kuwa thamani ya shilingi imeshuku kwa kipindi cha mwaka
2014-2015 kutokana na kuimarika kwa dola na viwango fedha tofauti na shilingi hivyo ni vyema ukawepo uthibiti wa fedha za kigeni na
uongezaji thamani ya mauzo yanayofanywa nje ya nchi.
Katika hatua
nyinge serikali leo imetoa ufafafauzi kuhusu hatua zilizochukuliwa kufutia
kitendo cha uzalilishwaji mwanafunzi mtanzania anayesoma nchini india ambapo
waziri wa mambo ya Nje Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk.
Augustino Mahig amesema kuwa ubalozi wa Tanzania Nchini India umekutana na uongozi wa wizara ya
mambo ya nje inchini humo na kuhakikisha
kuwa wote walitekelaza vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria na
serikali ya nchi hiyo imeahidi kutoa ulinzi kwa watanzania wanafunzi wanaosomea
kozi mbalimbali nchini humo.
No comments:
Post a Comment