Monday, April 25, 2016

IBADA YA JPILI TAR 24 APRIL 2016.


Nabii Mkuu Muheshimiwa Dr.GeorDavie ametangaza siku  ishirini na moja za kufuta kila aina ya maneno mabaya yaliyotamkwa kinyume kwa watu wote wanaomuamini Nabii,Na kusema kuwa
watu wote walioweka mizigo mabalimbali juu ya watu wa Mungu Mizigo hiyo imrerudi kwao.Nabii Mkuu ameyasema hayo katika ibada ya jiji iliyofanyioka katika chuo kikuu cha Manabii Kisongo Arusha Tanzania ambapo maelfu ya wakazi wa ndani na nje ya jiji la Arusha wamehudhuria pamoja na wengine kutoka mikoani na  nchi mbalimbali kama Kenya na Uganda.


Pia katika ibada hiyo Nabii Mkuu amewajenga watu na kuwataka kuwa imara siku zote hata asipokuwepo katika hema hilo,Sambamba na hayo amewafungua watu mablimbali na kuwatamkia matamko yenye uvuvio wa kinabii wa kuwapa upenyo mablimbali katika maisha yao.

Kadhalika ametamka matamko mbalimbali ya kufungua milango ya kifedha na kusema kuwa katika mwenzi mmoja na nusu kila utakachokigusa katika shughuli mbalimbali fedha itaonekana,

Hata hivyo watu mablimbali wemeshukuru sana na kuongelea vyema ibada hii yakipekee na kusema kuwa wanamshukuru Mungu kwa Neema hii ya kipekee ya kuwa na Nabii Mkuu Katika nchi ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment