Monday, December 10, 2018

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE AONGOZA IBADA YA MWISHO KWA SILVER PARTNERS.



KUTOKA KATIKA IBADA YA JIJI, CHUO KIKUU CHA MANABII, ILIYOFANYIKA KATIKA HEMA LA KUKUTANIA NGURUMO YA UPAKO, KISONGO, ARUSHA..
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie aliongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii siku ya jana ambapo ilikuwa ni ibada ya Silver Partners ya mwisho kwa mwaka huu wa 2018, ambapo aliweza kutamka baraka mbalimbali kwa wana-Silver Partners wote.
Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya watu Nabii Mkuu alifundisha somo lenye kichwa kisemacho "Kingdom Business" ambapo alisema kuwa mwili ni hekalu la Mungu na hekalu au Ufalme siku zote unahitaji kutunzwa hivyo kuwataka watu kama jinsi ambavyo walivyo na utamaduni wa kuvalisha miili yao bila kibali basi nguvu hiyo pia waitumie katika ku-support kazi ya Mungu na kutunza madhabahu.
Lakini pia Nabii Mkuu ametangaza kuwepo tena siku ya ijumaa ya week hii ya 14/12/2018 katika hema la kukutania kuanzia majira ya saa saba mchana ambapo itakuwa ni siku ya International Partners (IP), siku ambayo watu huwasilisha michango yao kwa ajili ya kuchangia GeorDavie Tv mbele ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.
 



NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

No comments:

Post a Comment