Monday, December 17, 2018

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE ATOA ZAWADI YA PESA KATIKA MTANDAO WA KIJAMII..


Wakati akitambuliwa kama Mtumishi wa Mungu mtoaji zaidi, Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amezidi kudhihirisha hilo kwa kuzidi kutoa misaada na zawadi mbalimbali kwa watu wote (Wanangurumo na wasiokuwa waumini wa Ngurumo Ya Upako).
Ni katika mtandao wa kijamii ujulikanao kama Facebook ambapo Nabii Mkuu alitoa zawadi ya Tsh,100,000 kwa Cosmas Mlingi baada ya kupendezwa na jinsi alivyo-comment katika moja ya post iliyopo kwenye account yake yenye jina la "GeorDavie Royal Mkuu".
Kijana huyo aliweza kuandika maneno mazuri yaliyowagusa watu wengi akimuelezea Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie na Nguvu ya Mungu aliyokuwa nayo kama unavyoweza kuona pichani.
Wakizungumzia tukio hilo watu wachache kati ya wengi tuliopata nafasi ya kuzungumza nao, wameelezea namna wanavyojivunia kuwa na Baba wa Kiroho kama Nabii Mkuu ambaye amekuwa kama Baba wa kimwili pia kutokana na upendo alionao na moyo wa kipekee katika kusaidia watu.
Pia wamewataka watu kubadilika na badala ya kuandika vitu visivyo na maana katika post za Watumishi wa Mungu waanze kuandika vitu vizuri, vyenye maana na akili ambavyo vinaweza kuwajenga na wengine wasioamini, na kusema pia Neema ya Kinabii ipo kwa anayejitambua na humfikia kila anayefanya jambo zuri kwaajili ya Serikali Tukufu ya Ufalme wa Mungu kwa njia nyingi zisizotarajiwa.
NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

No comments:

Post a Comment