Thursday, February 20, 2014

Rais wa Ukraine akubali kufikia makubaliano na upinzani

Rais  wa  Ukraine Viktor Yanukovich  ametangaza makubaliano  na  viongozi  wa upinzani  na  kuanza majadiliano  kumaliza  umwagikaji  wa  damu. Taarifa  hiyo imekuja  baada  ya  mkutano  pamoja  na  viongozi  watatu wa  upinzani, Vitali Klitschko, Arseny Yatseniuk  na mwanasiasa  mwenye mtazamo  wa  kizalendo anayefuata siasa kali  za mrengo  wa  kulia Oleh Tyahnibok. Wakati huo  huo rais  wa  Marekani  Barack  Obama  ametuma ujumbe  kwa  serikali  ya  Ukraine  kushughulikia  ghasia zinazotokea  nchini  humo  za  kuipinga  serikali  kwa  njia ya  haki.Watu  26  wameuwawa  katika  ghasia  za  mitaani  mjini Kiev  tangu  Jumanne. Tovuti  ya  rais  imetangaza   kuwa polisi  hawatavamia makambi  ya  waandamanaji  katika uwanja  wa  Uhuru  kama  ilivyopangwa . Katika  hatua nyingine  jana  jioni, rais alimbadilisha  mkuu  wa  jeshi  la Ukraine. Katika  mkutano  wa  pamoja  na  waandishi habari  mjini  Paris  jana  Jumatano kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel  na  rais  wa  Ufaransa  Francois  Hollande wametoa  wito  wa  kuwekwa  vikwazo  maalum  dhidi  ya uongozi  wa  Ukraine. Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa Ujerumani  Frank-Walter Steinmeier  atajiunga  na wenzake  wa  Ufaransa  na  Poland  mjini Kiev leo Alhamis.

No comments:

Post a Comment