Monday, February 17, 2014

(NEWS). UJERUMANI WAKIRI KUONGEZA UIMARA WA KIJASUSI DHIDI YA NCHI ZA MAGHARIBI.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya jarida la kila wiki la Ujerumani, Der Spiegel.Ripoti hiyo inasema balozi za nchi za magharibi kama vile Marekani na Uingereza hapa Ujerumani zitafuatiliwa kwa karibu zaidi.
Kwa sasa Ujerumani huzifuatilia kwa karibu nchi kama vile Urusi na China, lakini haizilengi nchi zilizo washirika wake kwa kiwango kama hicho.
Inafikiriwa kwamba simu ya kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ilifuatiliwa kutoka ubalozi wa Marekani mjini Berlin.

Jarida la Spiegel linasema mipango hiyo inafuatia ufichuzi wa udukuzi wa kiwango kikubwa uliofanywa na shirika la usalama wa kitaifa la Marekani, NSA.

No comments:

Post a Comment