(NEWS). MADEREVA WA BENAKO WILAYA YA NGARA WALIA NA KUMALIZIWA KWA EGESHO LA MAGARI
Baadhi ya madereva katika mji mdogo
wa Benako Wilayani Ngara mkoani Kagera wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo
kukamilisha ujenzi wa kituo cha kuegesha magari kilichoanza kujengwa tangu
miaka mitatu iliyopita kwenye eneo hiloWakiongea na N.Y.U Radio madreva hao
wamesema wanapata shida katika kusafirisha na kushusha abiria kutokana na
kuwepo msongamano wa magari makubwa yanayokwenda na kutoka katika nchi za
maziwa makuu.Mmoja wa maderva hao amesema kuwa
kituo cha kuegesha magari katika mji wa benaco kiliwekewa jiwe la msingi katika
mbio za mwenge kitaifa mwaka juzi lakini
hadi kufikia sasa wananchi hawaoni
kinachoendelea katika ujenzi huo. Aidha Diwani wa kata ya kasulo Dr
Philbert Kiiza amesema ucheleweshwaji wa kujenga kituo hicho umechangiwa na
wenye viwanja katika eneo la ujenzi kutojenga makazi kwa kufuata taratibu za
mipango miji katika kata humo.
No comments:
Post a Comment