Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie ametoa gari jipya aina ya Honda station wagon yenye namba za usajili T169 EEP kwa muandaaji wa mashindano ya Miss Tanzanite Manyara Bi. Aminata pamoja na shilingi milioni 11.4.
Monday, November 27, 2023
NABII MKUU DKT.GEORDAVIE AKABIDHI GARI NA SHILINGI MIL 11.4 KWA MUANDAAJI YA MISS TANZANITE MANYARA.
NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE AISHUKURU SERIKALI KWA KUMPA BARABARA.
Nabii Mkuu Mhe Dkt.GeorDavie ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wake katika jamii na kumpa heshima ya kuandika jina lake na huduma yake kwenye barabara mbili hapa jijini Arusha ambapo kuna barabara ya GeorDavie Road na Ngurumo ya Upako Road.
Friday, November 17, 2023
NABII MKUU DKT. GEORDAVIE KUPANDISHA VIWANGO VYA WATU KIMAISHA.
Nabii Mkuu Mheshimiwa Dkt.GeorDavie Balozi wa Amani anatarajia kupandisha viwango vya watu kimaisha ili waondokane na umasikini.
NABII MKUU KUPOKEA ZAWADI ZA PONGEZI JUMAPILI HII NOV 19, 2023
Nabii Mkuu Mheshimiwa Dkt.GeorDavie anatarajia kupokea zawadi za pongezi kwa kuanzisha Ngurumo ya Upako Radio ( N.Y.U. FM 99.3 MHz) kutoka kwa watoto wake wa kiroho.
Nabii Mkuu atapokea pongezi hizo ambazo ni kwa mfumo ya fedha katika ibada ya chuo kikuu cha manabii itakayofanyika jumapili katika nyumba ya matamko Ngurumo ya Upako Kisongo jijini Arusha ambapo itakuwa ni ibada ya kupanda viwango kimaisha.Akizungumza kuhusu Radio Kadinali wa kwanza wa huduma ya Ngurumo ya Upako Mtume Gaudensia Luila amesema kuwa siku tutamshukuru Mungu kwa ajili ya radio ambayo imefanyika Baraka na msaada mkubwa kwa watu wengi ambapo kupitia radio watu wamepomea uponyaji, mitaji na Baraka mbalimbali za kiroho na kimwili.
Amesema tunapomshukuru Mungu kwa ajili ya radio pia ni wajibu wetu kumpongeza Nabii Mkuu ambaye ndiye muanzilishi na msimamizi wa Radio.
Aidha katika ibada hiyo kila mtu atapata nafasi ya kusapoti Radio pamoja na kumpongeza Nabii Mkuu kwa mambo mengi anayoyafanya kwa watu bila mbalimbali kubagua na huduma kwa ujumla.
Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA.
Tuesday, November 14, 2023
DKT.GEORDAVIE" FEDHA INAPATIKANA KWA KUFANYA KAZI KWA BIDII."
Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie amewataka watu kutambua kuwa fedha inapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa na akili yenye ufahamu.
Monday, November 13, 2023
NABII MKUU" ACHA KULIPIZA KISASI SAMEHE UISHI KWA AMANI NA FURAHA."
Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie Balozi wa Amani amewataka watu kuacha tabia ya kulipiza kisasi kwa watu waliowakosea na badala yake wawe watu wa kusamehe ili waweze kupokea Baraka zao kutoka kwa Mungu.
Saturday, November 11, 2023
NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE ANATARAJIA KUONGOZA IBADA YA JUMAPILI YA KESHO NOV12, 2023
Nabii Mkuu Mhe. Dkt.GeorDavie kesho jumapili anatarajia kuwaongeza maelfu ya watu kiuchumi kupitia ibada ya chuo kikuu cha manabii itakayofanyika katika nyumba ya amtamko ngurumo ya upako kisongo Arusha.
Sunday, November 5, 2023
NENO LA WIKI HII KINABII KWA AJILI YAKO KUTOKA KWA NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE
Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie ametanga neno la wiki hii kuwa hii ni wiki ya kukumbukwa kwa maombi yako.
Ametanga neno hilo jumapili ya tarehe 05.11.2023 katika ibada
iliyofanyika nyumba ya matamko kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni ibada ya
kukumbukwa kwa maombi yako.
Nabii Mkuu amesema kuwa kila jambo ulilowahi kuomba kwa wakati wowote ule wiki hii linakumbukwa huku akiongeza kuwa wiki hii imekuwa ni kumbukumbu mbele ya Mungu kwa ajili ya maombi yako ili kila jambo liweze kujibiwa.
Na Deogratius Festo.
Thursday, November 2, 2023
NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE AWAFUTIA MAELFU YA WATU MAPIGO MATATU ADUI ALIYOKUSUDIA KUWADHURU
Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie Balozi wa amani amewafutia maelfu ya watu mapigo matatu ambayo adui alikusudia kuwadhuru watu wa Mungu.
Nabii Mkuu amefuta mapigo hayo ambayo ni ajali, kifo cha ghafla na janga la uharibifu kupitia kipindi maalum kilichorushwa live kupitia N.Y.U Radio jumatano usiku ambapo Mungu alimpa dhamana ya kufutia watu mapigo hayo.
Akitamka matamko ya kufuta mapigo hayo Nabii Mkuu amesema kuwa Mungu amekukusudia kupokea uzima na uhai na watu wamepokea amani, kuwa salama na kuwa vyema.
Akizungumza katika kipindi hicho Nabii Mkuu amesema kuwa jambo kama hilo haliwezekani kwa maombi bali linamuhitaji Nabii Mkuu ili kutoa maelekezo.
Aidha watu walipata nafasi ya kutuma sadaka zao maalum za kuepuka mapigo yote matatu ya adui sawasawa na maagizo ya Nabii Mkuu.
Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA.
Tuesday, October 31, 2023
BREAKING NEWS: NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE KUWEPO REDIONI' JUMATANO HII NOV 01, 2023
Monday, October 30, 2023
NENO LA KINABII WIKI HII KUTOKA KWA NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE
NABII MKUU DKT. GEORDAVIE: NAKUTAMKIA KUPOKEA WIKI YA HEKIMA NA UFAHAMU!!
Aidha utajiungamanisha na neno hilo la wiki hii kwa kutuma sadaka yako jumanne na alhamisi kuanzia shilingi 5,000/= na kuendelea na mara baada ya kutuma sadaka yako kupitia namba hizi 0769 00 00 34 / 0788 00 00 35 utaandika maneno yafuatayo;
JUMANNE: HEKIMA
ALHAMISI: UFAHAMU
NABII MKUU DKT. GEORDAVIE "HEKIMA NA UFAHAMU NI CHANZO CHA KUMJUA MTAKATIFU WA MUNGU"
Nabii Mkuu Mheshimiwa Dkt.GeorDavie amesema kuwa mtu anaweza kuwa na hekima lakini akakosa ufahamu.
Nabii Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akifundisha katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni iabada ya kupokea hekima na ufahamu.
Akifundisha kuhusu somo lililokuwa na kichwa kisemacho kumjua mtakatifu ni ufahamu Nabii Mkuu amesema kuwa kumjua aliyechaguliwa na Mungu, kumjua mteule aliyebeba kusudi la wakati au majira ni ufahamu.
Pia Nabii Mkuu ameitangaza wiki hii kuwa ni wiki ya kupokea hekima na ufahamu.
Na Beatrice Maina.