Huduma
ya Ngurumo ya Upako iliyoko chini ya Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie leo imetoa
msaada kwa vituo sita vya watoto yatima wenye thamani ya shilingi milioni kumi
.
Msaada
huo ambao ni vitu mbalimbali kama Mchele, sukari, mafuta ya kupikia pamoja na
sabuni umekabidhiwa kwa walezi wa vituo hivyo lengo likiwa ni kuwasaidia watoto
hao ili nao wajione kuwa sawa na watoto wengine wenye wazazi.
Akikabidhi
misaada hiyo kwa niaba ya Nabii Mkuu, Kadinali wa Kwanza wa Huduma ya Ngurumo
ya Upako Mtume Gaudensia Luila amesema kuwa misaada hiyo ni kutimiza neon la bwana.
Akipokea
msaada huo Mkurugenzi wa kituo cha watoto cha Lohada ameishukuru huduma ya
Ngurumo ya upako kwa kumpatia msaada kwa ajili ya watoto.
Kwa
upande wao walezi wa vituo hivyo wameonyesha furaha wakipokea msaada huo huku wakitoa wito kwa
jamii, serikali na taasisi mbalimbali kuweza kutoa michango yao ili kuweza
kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
No comments:
Post a Comment