Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha
miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na
uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono.
Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo.
Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.
wafuasi wa bwana Bemba wakifuatilia hukumu yake kutokea DRC
Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.
No comments:
Post a Comment