Akizungumza
jijini, Dar es Salaam jana, Ummy alitolea ufafanuzi kuhusu ugonjwa huo
na kuongeza ndani ya wiki moja, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa 11 na
kufanya jumla ya wagonjwa kufikia 32, ingawa idadi ya vifo
haijaongezeka.
Alisema
majibu kuhusu ugonjwa huo yanatokana na uchunguzi wa awali uliofanywa
na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na kwamba serikali imechukua
nafaka kadhaa zinazopatikana mkoani Dodoma ili kuzipeleka Atlanta,
Marekani kwa uchunguzi zaidi.
“Tulitoa
taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo Juni 19 mwaka huu ambao ulipatikana
wilaya za Chemba na Kondoa, kulikokuwa na wagonjwa 21 na vifo saba, hata
hivyo mpaka kufikia juzi wagonjwa waliokumbwa na ugonjwa huo
wameongezeka na kufikia 32 na idadi ya vifo imebakia saba,” alisema Ummy.
Alisema
katika jitihada za kutambua kiini cha ugonjwa huo, Wizara imepeleka
jopo la wataalamu huko Dodoma ili waweze kushirikiana na wenzao walioko
huko kufanya uchunguzi wa kina wa ugonjwa huo.
Alisema
sampuli mbalimbali za damu, haja ndogo, haja kubwa, vinyama vya ini na
sampuli za vyakula, zilipelekwa katika maabara za Mkemia Mkuu wa
Serikali, maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Maabara ya Taifa
ya Magonjwa ya Binadamu na maabara ya Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya
Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Vile
vile sampuli nyingine kesho zitapelekwa Marekani katika maabara ya
Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Marekani (CDC) kilichopo Atlanta kwa
uchunguzi zaidi,” alisema Ummy.
Aidha alisema, “kuna
uwezekano mkubwa kwamba ugonjwa huu umesababishwa na ulaji wa chakula
kilichokuwa na sumukuvu na kuleta madhara, ili kuwa na uhakika na jambo
hilo Wizara yangu inasubiri matokeo ya vipimo vya damu na haja ndogo
vilivyopelekwa katika Maabara ya CDC matarajio yetu ni kupata majibu
hayo katika kipindi kisichozidi wiki moja.”
Alisema tangu ugonjwa huo ulipoibuka, wagonjwa 12 wametibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na 18 wametibiwa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
Alisema tangu ugonjwa huo ulipoibuka, wagonjwa 12 wametibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na 18 wametibiwa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
No comments:
Post a Comment