Tuesday, June 21, 2016

WABUNGE UPINZANI WAENDELEA KUGOMEA VIKAO VYA BUNGE, LEO WATOKA KIMYAKIMYA

Wabunge wa Ukawa wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Dk Tulia Ackson, lakini leo wametoka kimyakimya bila mbwembwe kama za jana.

Kwa sasa kamati ya uongozi ya umoja huo imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema watatoa taarifa kamili baada ya kumaliza kikao hicho.

No comments:

Post a Comment