Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema watu hao waliuawa
Jumanne Desemba 5,2017 jioni katika msitu wa Njoro wakati wa majibizano
ya risasi na polisi.
Amesema
watuhumiwa hao wa ujambazi walikuwa wakiishi chumba kimoja eneo la
Njoro ambako polisi walipofika hawakuwakuta na walipata taarifa kuwa
wamejificha msituni.
Kamanda
Issah amesema kwa kushirikiana na wananchi walikwenda ndani ya msitu
huo ambako walisikia milio ya risasi ndipo askari walipofyatua risasi na
kusababisha vifo vyao.
Amewataja
waliouawa kuwa ni Yusufu Juma Mdoe aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya
mauaji mwaka 2015; Francis Hamis Kinyaia ‘Wakudata’ ambaye amesema
alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji mwaka 2013.
Kamanda Issah amemtaja mwingine kuwa ni Valerian Joackim ‘Mdoe’ aliyekuwa na kesi ya mauaji ya mwaka 2013.
Amesema
uchunguzi wa polisi umebaini watuhumiwa hao walihusika katika tukio la
kufungwa miguu, mikono na kuzibwa mdomo mlinzi lililotokea Novemba
24,2017 eneo la Uru Shimbwe. Katika tukio hilo, bunduki mbili aina ya
shotgun ziliporwa.
Kamanda
Issah amesema katika msitu wa Njoro walikuta bunduki moja aina ya
shotgun iliyokatwa mtutu na kitako, huku namba zikiwa zimefutwa, risasi
tatu, maganda matatu ya risasi, mapanga mawili, mkasi unaotumika kukata
makufuli, kirungu cha polisi, tindo na misokoto miwili ya bangi.
Ameema miili ya watuhumiwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.
No comments:
Post a Comment