Sunday, October 14, 2018

Kumbukizi ya Miaka 19 ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere



Oktoba 14, 2018 ni kumbukizi ya miaka 19 tangu afariki dunia
Mwasisi wa Taifa la Tanzania na mpigania Uhuru wa Tanganyika
 pamoja na mataifa mbalimbali barani Afrika, Hayati Mwl. Julius
Kambarage Nyerere.

Katika kumbukizi hii, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
mkewe Mama Janeth Magufuli wamemtembelea mjane wa
Mwl. Nyerere, Mama Maria Nyerere anayeishi Msasani Jijini Dar es salaam.
Mhe. Rais Magufuli amesema serikali itaendelea kumuenzi Baba
wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa fikra na mipango
mizuri aliyoiweka inatekelezwa kwa manufaa ya watanzania wote.
Hayati Mwl. Nyerere aliyezaliwa mwaka 1922, alifariki dunia Oktoba
14, 1999 akiwa nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama J
aneth Magufuli walimtembelea mjane wa Mwl. Nyerere,
Mama Maria Nyerere nyumbani Msasani Jijini Dar es salaam.
Mhe. Rais Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere.
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere.

No comments:

Post a Comment