Monday, February 4, 2019

ALIPIWA DENI, KODI NA MTAJI..

"Mungu amenikumbuka, ameniona na amenifuta machozi" ni kauli ambayo ilitolewa na mwanamama aliyesaidiwa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie baada ya kulipiwa kodi ya nyumba ya mwaka mzima pamoja na miezi mingine minne aliyokuwa akidaiwa ambapo pia aliongezewa mtaji wa biashara yake.
Mwanamama huyo anayefanya biashara ndogo ndogo alifika akilia mbele ya Nabii Mkuu ambapo alisema kuwa amekimbiwa na mume na kuachiwa watoto wanne, wakiwa wanaishi katika chumba kimoja ambacho alikuwa akidaiwa kodi ya miezi minne pamoja na watoto wake.
Baada ya kujieleza Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie alitoa pesa taslimu na kumkabidhi ili aweze kulipa kodi hiyo aliyokuwa akidaiwa pamoja na kumuongezea nyingine kwa ajili ya mwaka mzima ambapo alimuongezea mtaji wake ili aweze kujikimu na maisha.
Akizungumzia hilo Nabii Mkuu amesema kuwa Serikali Tukufu Ya Ufalme Wa Mungu imeamua kugusa matatizo ya kifedha waliyonayo watu wake ili kuhakikisha shida zinawapungukia na hatimaye kuisha kabisa.
Hayo yamejiri siku ya jana katika ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii, Ngurumo Ya Upako, ambapo ilikuwa ni ibada ya "Kufuta kumbukumbu zote mbaya maishani" ikiongozwa nae Nabii Mkuu.
Akizungumza katika ibada hiyo Nabii Mkuu alisema kumbukumbu mbaya hufanya watu wasipige hatua katika maisha, waishi wakiwa na huzuni pamoja na chuki ambapo alitamka matamko ya Kinabii kwaajili ya kuwatenganisha watu na hali hiyo.
Wakati huo huo Nabii Mkuu anatarajia kuwepo katika kipindi cha "Q and A AKILI KUBWA" siku ya leo kuanzia saa mbili na nusu za usiku, kipindi kitakachoruka kwa kupitia 99.3 N.Y.U Radio pamoja na GeorDavie Tv ambapo jumla ya 2,000,000 (milioni mbili) zitatolewa kwa washindi watakaoweza kujibu maswali kwa ufasaha kabisa.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

No comments:

Post a Comment