Thursday, March 28, 2019

AJENGEWA NYUMBA, WENGINE WASAPOTIWA FEDHA..

Kanisa dogo la mkoani Kilimanjaro lililopatiwa msaada na Nabii Mkuu.

Nyumba mpya anayojengewa Bi. Nawasa ikiwa inaendelea na ujenzi.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa msaada wa jumla ya sh. 2,300,000 (milioni mbili na laki tatu), kwa watu watatu tofauti huku mwingine akipata neema ya kujengewa nyumba.
Hayo yamejiri wiki hii baada ya Nabii Mkuu kuguswa kuwasaidia watu wawili tofauti mtaji wa sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kila mmoja kwa ajili ya kuwawezesha kupata mtaji wa kuanzisha biashara.
Kwa upande mwingine Mchungaji mmoja wa kanisa dogo mkoani Kilimanjaro (jina lake na la kanisa linahifadhiwa) amebarikiwa sh. 300,000 (laki tatu) mara baada ya Nabii Mkuu kuliona kanisa hilo la mbao (kama linavyoonekana pichani) wakati akipita na msafara wake na kuwakuta katika ibada yao ambapo aliguswa kushuka na kuwasapoti kifedha na kisha kuendelea na safari yake.
Mchungaji huyo pamoja na waumini wake wasiozidi kumi (10) wakizungumza mara baada ya kupokea baraka hiyo ya kifedha walionyesha furaha yao na kutoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kutokana na msaada huo.
Wakati huohuo mwanamke mmoja muumini wa huduma ya Ngurumo Ya Upako anayefahamika kwa jina la Nawasa Saibulu, amepata neema ya kipekee ya kujengewa nyumba na Nabii Mkuu (kama inavyoonekana pichani ikiwa inaendelea na ujenzi) baada ya nyumba ya awali aliyokuwa akiishi iliyokuwa ya udongo kuharibika na kuwa na tatizo la kuingiza maji kipindi cha mvua.
Mwanamke huyo ni miongoni mwa watu waliopata neema hiyo ya kuboreshewa makazi yao kwa mwaka huu wa 2019.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali ya kifedha ambapo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 ametumia zaidi ya sh. 40,000,000 (milioni arobaini) katika kugusa mahitaji mbalimbali ya watu kutoka sehemu tofauti tofauti duniani.


NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

No comments:

Post a Comment