Serikali
imelieleza bunge kuwa biashara ya kuni na mkaa ni halali,rasmi na haina
kizuizi kwa mwananchi yeyote ili mradi anafuata mwongozo wa uvunaji
wa mazao ya misitu wa mwaka 2007 na marekebisho yake ya mwaka 2015.
Hayo
yamesemwa Juni 10,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe.Costantine Kanyasu wakati akijibu swali la
mbunge wa viti Maalum Zubeda Sakuru aliyehoji ongezeko la gharama za
nishati nchini hasa umeme na gesi zimepelekea kuwa na ongezeko kubwa la
matumizi ya kuni na mkaa je,lini serikali itarasmisha biashara ya mkaa
ili kupunguza makali ya maisha.
Akijibu
Swali hilo,Mhe.Kanyasu amesema biashara ya kuni na mkaa inafanyika kwa
mujibu wa sheria na kanuni za misitu ,pamoja na tangazo la serikali
Na.324 la 14/08/2016 na mwongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa
mwaka 2007 uliofanyiwa marekebisho mwaka2015.
Kutokana
na hilo,Naibu Waziri Kanyasu amesema biashara ya kuni na mkaa ni rasmi
na haina kizuizi chochote kwa mwananchi na kinachotakiwa ni kufuata
sheria na taratibu za biashara za uvunaji wa mazao ya misitu.
Aidha,Mhe.Kanyasu
amezitaja baadhi ya taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa na kuzingatiwa
wakati wa kutaka kufanya biashara ya mkaa na kuni ni pamoja na kutenga
maeneo ya misitu kwa ajili ya kutengeneza mkaa,kusajiliwa na meneja wa
misitu wa wilaya,kutuma maombi ya usajili kwa afisa misitu wa wilaya na
kila mfanyabiashara kulipia mrabaha .
Hata hivyo,serikali imehimiza watanzania kuanzisha mashamba ya miti kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na nishati.
by Rich Voice.
No comments:
Post a Comment