Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema serikali yake tayari imenunua mtambo wa kujikinga na makombora kutoka Urusi.
Erdogan
amewaambia wanachama wa chama chake cha AKP kuwa mfumo huo wa kujikinga
na makombora utawasili Uturuki mwezi Julai mwaka huu.
Mpango
huo wa Uturuki kununua mtambo huo kutoka Urusi umekuwa kiini cha
mvutano na muungano wa kujihami wa NATO, ambao Marekani na Uturuki ni
wanachama.
Marekani na washirika wengine wa NATO wanahofia kuwa Urusi huenda ikazipeleleza ndege za NATO kwa kutumia mtambo huo wa S-400.
Ili
kuizuia Uturuki kufanya ununuzi huo, Marekani ilisitisha mpango wa
pamoja wa ndege za kivita aina ya F-35 na kuitishia Uturuki na vikwazo
zaidi vya kiuchumi.
No comments:
Post a Comment