KATIBU
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Bashiru Ally amezindua ujenzi wa
ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mkoani Pwani,ambapo amechangisha
zaidi ya milioni 25 na vifaa mbalimbali.
Katika
uzinduzi huo, jumla ya mifuko ya saruji 2,861 imechangiwa ,nondo tani
tano thamani ya milioni 9 ,malori ya mchanga, fedha taslimu ni
sh.milioni 22.562 na ahadi ni sh.milioni 2.5 .
Alisema kati ya fedha hizo milioni tano imechangiwa na mwenyekiti wa CCM Taifa dk.John Magufuli.
Bashiru
alisema, kwasasa hakuna mtindo wa kuchangia shughuli za kichama kwa
fedha za mikononi ili kuweka mifumo mizuri ya kuaminiana.
Aidha alisisitiza ujenzi wa ofisi za chama ili kukijenga chama kwa maslahi ya wanaCCM.
“Uhai
wetu unatokana na vikao na vikao haviwezi kufanyika chini ya miti,au
kukutana gesti ,hivyo jengeni ofisi za chama kuanzia matawi na kata ili
kuimarisha chama chetu”
Hata
hivyo aliwasihi wananchi wasiwasikilize wale wanaokebehi Chama
kilichopo madarakani na wale wanaopotosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.“Upotoshaji ni dhambi hasa kwa mtu aliyesoma chuo cha Dar es salaam na kusisitiza kwamba ,hali ya uchumi wetu ni imara” .
“Huwezi
kudanganya watu na kuwaona ni wa pumbavu ,hakuna uchumi uliokufa
,hatuna deni la ndege,tunajenga vituo vya afya ,tunatundika nishati ya
umeme hadi vijijini,watoto wanasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi
kidato cha nne leo mtu unaibuka anasema uchumi umekufa”alikemea Bashiru.
Hakusita
,kuupongeza mkoa kwa kushirikiana ,kushikamana na kuwa na mahusiano
mema baina ya serikali na chama. Aliweka wazi wilaya ambazo bado hazina
mahusiano mazuri kati ya serikali na chama ikiwemo Bagamoyo ,Rufiji na
Kibaha Vijiji ambako pale tatizo lipo kwa mkurugenzi mtendaji wa Kibaha
Vijijini.
Alimjia
juu mkurugenzi huyo wa wilaya ya Kibaha kwa kufanya kazi zake kwa
mazoea na kushindwa kujenga mahusiano na ushirikiano na chama na kwenye
majukumu yake ya kazi. Katika hatua nyingine akielekeza juu ya muelekeo
wa chaguzi zijazo ,Bashiru aliwataka viongozi wanaokaa kwenye vikao vya
maamuzi waache kutembea na wagombea mifukoni na badala yake waache
wabunge,madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa waliopo wafanye kazi.
Pia
aliwaasa baadhi ya wabunge kuacha kutumwa na kuwa wapiga debe kwa
wawekezaji uchwara bali waelekezeni wawekezaji masharti na taratibu za
nchi kwa maslahi mapana ya nchi.
SOURCES :CCM
No comments:
Post a Comment