Thursday, June 13, 2019

Thamani ya shilingi ya Tanzania yazidi kuimarika


Thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika na katika kipindi kinachoishia Aprili 2019, Dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Sh2,300.9 ikilinganishwa na Sh2,270.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.

Utulivu katika mwenendo wa thamani ya shilingi umetokana na utekelezaji wa sera ya fedha, usimamizi madhubuti wa mapato na matumizi ya Serikali, matumizi ya gesi asilimia badala ya mafuta na kuzalisha umeme.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango  wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa  mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.

“Sababu nyingine ni baadhi ya viwanda kuzalisha bidhaa ambazo awali zilikuwa zikiagizwa kwa wingi kutoka nje ikiwemo vigae na marumaru,” amesema Dk Mpango.

No comments:

Post a Comment