Friday, June 14, 2019

Uturuki kulipiza kisasi ikiwekewa vikwazo na Marekani


Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema nchi yake italipiza kisasi dhidi ya uwezekano wowote ule wa Marekani kuiwekea vikwazo nchi yake kutokana na makubaliano yake na Urusi ya kununua mfumo wa kukinga makombora aina ya S-400. 
Akiutetea ununuzi huo, Mevlut Cavusoglu ameliambia leo shirika la habari la serikali nchini Uturuki la Anadolu kwamba Uturuki kama taifa huru linaweza kuchagua vifaa vya ulinzi inavyovitaka. 
Ununuzi huo wa mfumo wa ulinzi kutoka Urusi umeharibu uhusiano kati ya washirika hao wawili wa jumuiya ya kujihami NATO. 
Marekani imesema mfumo wa huo wa ulinzi wa aina ya S-400 ni kitisho dhidi ya ndege zake za kivita za aina ya F-35. 
Marekani imeionya Uturuki kwamba kuna uwezekano ikaiwekea vikwazo iwap itapokea mfumo huo wa ulinzi kutoka Urusi.

No comments:

Post a Comment