Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ameendelea
kukubalika kimataifa baada ya Jarida maarufu Duniani la Forbes kubashiri
kwamba ataivusha Tanzania na kuwa nchi yenye kipato cha kati kupitia
ajenda yake ya Tanzania ya viwanda chini ya mpango wa maendeleo wa 2025.
Katika
jarida hilo la Forbes Afrika la Julai mwaka huu ambalo lilikuwa mahsusi
kwaajili ya kelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano na uongozi
wa Rais Magufuli kwa ujumla, imeelezwa maono yake kama kiongozi wan chi
yameifanya Tanzania kupiga hatua kubwa za maendeleo na inatarajiwa kuwa
miongoni mwa nchi chache sana za Afrika zenye maendeleo yanayoonekana
na yanayopatikana kwa muda mfupi.
Kwamujibu
wa Jarida hilo ambalo limemwelezea Rais Magufuli kama Tingatinga katika
kusimamia kile anachokiamini, miongoni mwa mambo makubwa yanayomfanya
ang’ae kimataifa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya standard Gauge
SGR, upanuzi wa bandari na ujenzi wa miundombinu ya barabara
zinazounganisha nchi nzima ambazo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo
hapa nchini.
Aidha
Rais Magufuli ameelezewa kuwa ni mtu asiye na masihara katika kusimamia
masuala ya maendeleo, mfano jinsi alivyosimamia na kuhakikisha uwanja
wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere terminal three unakamilika kwa
wakati na kwa kiwango cha kimataifa.
Jarida
la Forbes limeendelea kumwelezea Rais Magufuli kuwa, mafanikio mengi
anayopata ni kutokana na kuongozwa na mpango wa maendeleo wa 2025
pamoja na ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015.
Miradi
mingine iliyoainishwa kuonyesha utendaji wake ni ile ya umeme ya
Kinyerezi awamu ya kwanza ya pili nay a tatu, pamoja na mradi mkubwa wa
kuzalisha umeme katika maporomoko yam to Rufiji maarufu kama Stieglers
Gorge,ambayo lengo lake ni kumaliza kabisa tatizo la umeme hapa nchini
hasa kwa wananchi wa vijijini.
Kuhusu
ukuaji wa uchumi Jarida la Forbes limeelezea kuwa katika kipindi cha
utawala wake tangu aingie madarakani mwaka 2015, uchumi umeendelea kukua
kwa kasi kwa kiwango cha asilimia 7 ambao ni ukuaji wa mfano na
wakuridhisha kwa nchi za Afrika ikilinganishwa na miaka mingi
iliyopita.
Katika
uwekezaji Rais Magufuli amenukuliwa akiwahakikishia wawekezaji na dunia
kwa ujumla kwamba, Tanzania ni nchi salama na kwa uwekezaji na
akawakaribisha kuja kuwekeza kwani ameendelea kufanya mapinduzi makubwa
katika uwekezaji lengo kuu ikiwa ni kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
Mahojiano
ya Rais Magufuli yaliyotolewa na Jarida la Forbes Africa, yalifanyika
mapema mwaka huu ambapo Jarida hilo lilikuwa na toleo maalum la Tanzania
kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.
Credit: Michuzi
No comments:
Post a Comment