UJUMBE
wa Viongozi wa Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO wakiongozwa na
Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Roque Silva Samuel wakipewa maelezo
katika Eneo la Kihistoria alipouawa kwa kupigwa Risasi na Wapinga
Maendeleo Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume
April 7, Mwaka 1972.
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi(kushoto)
akikabidhiwa Tisheti na Katibu Mkuu wa Chama Chama Tawala cha Msumbiji
cha FRELIMO Ndugu Roque Silva Samuel(kulia) tukio hilo ikiwa ni ishara
ya kuendeleza ushirikiano na Urafiki kwa Vyama hivyo vyenye Historia
kubwa ya Urafiki wa Ukombozi wa Nchini mbali mbali za Afrika,ambapo
Hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo Tarehe
16/06/2019
KATIBU
Mkuu wa Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO Ndugu Roque Silva
Samuel(kulia),akimvisha Kofia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dk.Abdulla Juma Mabodi ikiwa ni ishara ya Ushirikiano wa kiutendaji
baina ya CCM na FRELIMO.
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akivishwa Kofia ya
FRELIMO na ATIBU Mkuu wa Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO Ndugu
Roque Silva Samuel, ikiwa ni ishara ya Ushirikiano wa kiutendaji baina
ya CCM na FRELIMO.
UJUMBE
wa Chama Tawala cha Msumbiji FRELIMO wakiongozwa na Katibu Mkuu wa
Chama hicho Ndugu Roque Silva Samuel wakiwa na Viongozi wa CCM na
Jumuiya zake katika eneo la Kaburi ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar
Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume wakiomba Dua.
……………….
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma
Mabodi,amesema Urafiki wa Vyama vya ASP,TANU na hivi sasa CCM na Chama
Cha Tawala cha Msumbiji FRELIMO ni wa Kihistoria uliodumu kwa muda
mrefu.
Alisema
Urafiki huo umefikia kiwango cha kuwa na uhusiano wa Kindugu na Kidamu
baina ya Wananchi wa Nchi hizo mbili,sambamba na kudumisha ushirikiano
katika nyanja za Kisiasa na Kidiplomasia.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akizungumza na Ujumbe wa Chama cha FRELIMO
ukiongozwa na Katibu Mkuu wake Ndugu Roque Silva Samuel, aliyefika
katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo ya
kuimarisha mahusiano baina ya Taasisi hizo za Kisiasa.
Dk.Mabodi
alisema Chimbuko la Urafiki kati ya Vyama hivyo umetokana na harakati
za Vyama vya ASP,TANU na FRELIMO vilivyoongoza harakati za Ukombozi
Barani Afrika na baada ya Nchi mbali mbali kupata Uhuru wa kujitawala
zenyewe viliendelea kuaminiwa na Wananchi wakavipa ridhaa ya kuongoza
Dola.
Alisema
kuwa Wananchi wa Msumbiji wanaishi kwa Amani na Utulivu Zanzibar na
wapo Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara wanaoishi Msumbiji kwa Amani
masuala yanayotakiwa kuenziwa ili Mahusiano hayo yawe imara zaidi kwa
maslahi ya Vizazi vya sasa na Vijavyo.
Katika
maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo alisema Rais wa kwanza wa Zanzibar
Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume aliongoza Mapinduzi ya Zanzibar ya
Mwaka 1964 na Zanzibar ikawa Huru za kuanza kujitawala yenyewe, ambapo
kwa sasa Nchi inaendeleza Mapinduzi ya Kiuchumi kupitia Sera zake imara
zilizowekwa na Chama Cha Mapinduzi.
Dk.Mabodi
alimwambia Katibu Mkuu huyo kuwa CCM itaendeleza Ushirikiano uliotukuka
ulioachwa na Viongozi Wakuu wa Nchi hizo za Msumbiji na Tanzania ambao
ni Marehemu Abeid Amani Karume,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere na
Hayati Samora Machel.
Naye
Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha Msumbiji Ndugu Roque Silva
Samuel,alishukru kwa mapokezi mazuri aliyopata Zanzibar na kueleza kuwa
lengo la ziara hiyo fupi ni kuishukru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa Msaada waliotoa hivi karibu wakati Msumbiji ilipokumbwa na
Maafa.
Alisema
Msumbiji ilipata Maafa ya Kimbunga mara mbili na kusababisha Vifo vya
Wananchi zaidi ya 600 na kuharibika kwa miundombinu ya Maakaazi,Shule
300,Barabara,Mawasiliano na Nyumba za Umma na binafsi.
“Tunawashukru
sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein kwa msaada wao Mkubwa waliotoa kwa Msumbiji kwani wameonyesha kwa
Vitendo namna wanavyojali
Katibu
Mkuu huyo wa FRELIMO alisema Chama hicho kimeendelea kufanya Siasa Huru
zinazojali Hali za Watu wote bila ubaguzi wa kabila,rangi na kidini.
Alisema
kwa sasa Msumbiji wanajiandaa na Uchaguzi Mkuu wa Dola unaotarajiwa
kufanyika Octoba 15,Mwaka 2019,Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa wa huru na
haki unakwenda sambamba na Matakwa ya Kidemokrasia.
No comments:
Post a Comment