Serikali
imeeleza kuwa inatarajia kuja na utaratibu mpya wa kutibu ugonjwa wa
Dengue ambao umezuka katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Dar es Salaam
na kupelekea vifo kwa baadhi ya watu na wengine kuugua.
Kauli
hiyo ya Serikali imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri Ummy Mwalimu
wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye alihoji juu
ya Serikali kugawa dawa mpya zitakazomaliza mbu wa ugonjwa wa Dengue.
Akiuliza
swali hilo Bungeni, Mbunge Zungu amesema kuwa, "bado kuna changamoto
kwenye upambanaji wa Dengue, Serikali itabadilisha dawa zinazotumika ili
wananchi washiriki wazimwage kwenye maeneo yao, Mheshimiwa Naibu Spika
ni kwamba sasa hivi Mbu wa Dengue wameanza kuingia kwenye daladala".
Akijibu
swali hilo Bungeni, Waziri Ummy amesema "suala hili limeanza kufanyiwa
kazi na Serikali, ndani ya siku 2 tutatoa kauli rasmi jinsi gani
tumechukua hatua za kupambana na Dengue".
"Niwaambie pia wananchi hakuna njia nyingine ya kujikinga na ugonjwa Dengue zaidi ya kuwatokomeza mbu hao," ameongeza.
No comments:
Post a Comment