Msemaji
wa makao makuu ya jeshi la Iran, Meja Jenerali Ebulfazl Shikarchi
amesema shambulizi lolote la kijeshi kutoka kwa Marekani litajibiwa
vikali kwa wao kushambulia maslahi ya Marekani katika eneo hilo pamoja
na kushambulia washirika wa Marekani.
Shikarchi akiongea na shirika la habari la Tesnim alitoa onyo kuhusiana na matokeo ya kuishambulia Iran kijeshi.
Shikarchi alisema hawatakuwa waanzilishi wa vita dhidi ya nchi yeyote lakini watakaposhambuliwa watajibu mapigo vikali mno.
Asubuhi
ya Alhamisi iliyopita, Ofisi ya Mahusiano ya Jeshi la Walinzi wa
Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ilitangaza habari ya kusambaratishwa ndege
ya ujasusi ya Kimarekani, baada ya ndege hiyo kukiuka anga na ardhi ya
Iran katika eneo la Kouh-e-Mobarak katika mkoa wa Hormozgan.
Komandi ya jeshi la Marekani katika eneo la Asia Magharibi (CENTCOM) sambamba na kukiri habari hiyo ilidai kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ya Marekani ilikuwa bado haijaingia katika anga ya Iran na kwamba ilikuwa katika maji ya kimataifa.

BY RICH VOICE
No comments:
Post a Comment