Friday, June 14, 2019

Shambulizi la meli ya mafuta katika Ghuba: Iran yasema madai ya Marekani hayana msingi


Iran imesema kuwa imepuuzilia mbali madai ya Marekani kwamba ndio iliotekeleza shambulio dhidi ya meli mbili za mafuta katka Ghuba ya Oman.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo aliilaumu Iran kwa kutekeleza shambulo hilo siku ya Alhamisi.

Aliongezea kwamba Marekani iliamua kuchukua uamuzi huo kutokana na ujasusi kuhusu silaha zilizotumika .Lakini Iran ilipinga madai hayo kama yasio ya msingi. 

Makumi ya wafanyikazi wa meli hizo waliokolewa baada ya milipuko hiyo katika meli zinazomilikiwa na Japan ya Kokuka Couregeous na Front Altair inayomilikiwa na kampuni ya Norway.

Katika taarifa iliotolewa siku ya Ijumaa, Ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa ulisema: Iran inapinga madai hayo ya Marekani ikizingatia shambulio la tarehe 13 mwezi Juni na kulishutumu kwa hali na mali.

Muda mfupi baada ya kukana , ofisi kuu ya jeshi la Marekani lilitoa kanda ya video iliosema inaonyesha jeshi la Iran la IRG likitoa bomu ambalo halikulipuka kandakando ya meli ya Kokuka Courageous kufuatia shambulio hilo.

Mlipuko huo unajairi mwezi mmoja baada ya meli nne za mafuta kuharibiwa katika shambulio ambalo halijadaiwa kutekelezwa na upande wowote katika bahari ya UAE . Wakati huo Marekani iliilaumu Iran -lakini Tehran ilikana madai hayo.

Bei ya mafuta ilipanda kwa asilimia 4 baada ya kisa hicho cha Alhamisi katika Ghuba ya Oman, ambayo iko katika eneo moja muhimu la meli ambapo mamia ya madola ya mafuta yanapitia.

Muungano mkubwa wa meli duniani BIMCO, umesema kuwa hali ya wasiwasi katika eneo hilo iko juu licha ya kuwa hakuna vita vinavyoendelea.

Wakati huohuo waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza alionya kuwa iwapo Iran imehusika- ni hatari kwa udhabiti na usalama wa eneo hilo

"Ni maono ya Marekani kwamba taifa la Iran linahusika na shambulio hili" , alisema Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo katika mkutano na vyombo vya habari mjini Washington.

"Uchunguzi huo unatokana na ujasusi , silaha zilizotumika, utaalamu wa hali ya juu uliotumika kutekeleza shambulio hilo, mashambulio kama hayo yaliotekelezwa na Iran katika siku za hivi karibuni dhidi ya meli na ukweli kwamba hakuna kundi linlotekeleza operesheni zake katika eneo hilo linaweza kutekeleza shambulio hilo kwa kiwango cha juu .

Hatahivyo Pompeo hakutoa ushahidi wowote.

''Hili ni shambulizi la hivi karibuni miongoni mwa msuuru wa mashambulio yaliotekelezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na washirika wake dhidi ya Marekani na washirika wake. Mashambulio hayo ynayonyesha wazi tishio la amani na usalama wa kimataifa-ikiwa ni unyanyasaji wa biasharavza meli mbali na kuwa ni kampeni isiokubalika inayosababisha hali ya wasiwasi'', alisema Pompeo.
Credit:BBC

No comments:

Post a Comment