*
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia kijana mweye umri
19 Ernest Joseph kwa tuhuma za mauji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Kimataifa cha Kampala (KIU) kilichopo Gongolamboto jijini Anifa
Mgaya(21).
Kijana
huyo anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo tayari amekiri kuhusika na
ameliambia Jeshi la Polisi kuwa baada ya kufanya tukio hilo la mauaji
kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kulia alichukua simu aina ya Tekno
na fedha Sh.8000 ambazo zilikuwa kwenye pochi.
Akizungumza
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo amefanya tukio
hilo la mauaji Juni 16 mwaka huu saa tatu usiku maeneo hayo ya Chuo cha
Kampala.
"Mtuhumiwa
amekiri kuhusika na mauaji ya mwanafunzi Anifa Mgaya (21) ambaye
alikuwa anasoma chuoni hapo ngazi ya Diploma.Mtuhimiwa alimchoma kisu
mwanafunzi huyo kifuani na kisha kuchukua simu ya Tekno na fedha
Sh.8000.
"Mwanafunzi
alifariki dunia muda mfupi baada ya kutokwa na damu nyingi, na
mtuhumiwa alikimbia baada ya kutenda kosa hilo.Jeshi la Polisi tuliahidi
kumsaka aliyehusika kokote aliko na jana tukamkata akiwa maeneo ya
Madale Mivumonijijini Dar es Salaam,"amesema Kamanda Mambosasa.
Akifafanua
zaidi kuhusu tukio hilo, Kamanda Mambosasa amesema katika mahojiano
mtuhimiwa amekiri kumchoma kisu na kueleza namna ambavyo Anifa alikuwa
amevaa siku hiyo kwa kueleza alikuwa amevaa fulana nyeusi , suruali ya
jinsi na kapelo.
"Mtuhumiwa
anaendelea kushikiliwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili,"amesema Mambosasa na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi
liliahidi kumsaka mtuhumiwa aliyehusika na mauji ya mwanafunzi huyo
kwani damu yake haijamwagika bure.
Wakati
huo huo Kamanda Mambosasa amesema kuwa wakati wa msako huo , wamekamata
wahalifu wengine 31 ambao wamekuwa wakifanya matukio ya uhalifu chuoni
hapo na kusababisha hofu kwa wanafunzi, ambao Polisi imeeleza kuwa
itaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na kisha sheria ichukue mkondo wake.
Mambosasa
amesema kuwa Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam litaendesha msako
kusaka wahalifu wote walioko kwenye maeneo ya vyuo na kufafanua yoyote
ambaye anajihusisha na matukio ya uhalifu atachukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment