Wanachama
883 wa Chadema wa kata ya Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
wamehama chama hicho na kujiunga na CCM wakimfuata mbunge wa jimbo hilo
James Ole Millya. Wanachama hao walirudisha kadi zao jana kwenye kijiji
cha Namaluli na kupokewa na katibu wa CCM wilayani Simanjiro Ally
Kidunda.
Akizungumza
baada ya wanachama hao kupokelewa Ole Millya alisema anawashukuru kwa
kuamua kumfuata CCM kwani awali walikuwa wote Chadema. Alisema yale
mambo waliyokuwa wanalalamika awali hivi sasa hayafanyiki hivyo wamuunge
mkono Rais John Magufuli ili wapatiwe maendeleo zaidi.
"Ninawashukuru
mno kwa ninyi kuja CCM kama mimi kwa ajili ya kumuunga mkono Rais
Magufuli mwenye maamuzi na moyo kama ya baba wa Taifa hayati mwalimu
Julius Nyerere wa kusimamia maendeleo," Katibu wa CCM wa wilaya ya
Simanjiro, Ally Kidunda aliwashukia vikali wanasiasa wanaoanza
kujipitishapitisha kwa wanachama wa chama hicho kufanya kampeni kabla ya
muda wa uchaguzi kufika.
Kidunda
alisema watawachukulia hatua kali wanachama hao kupitia vikao vyao
kwani yeye ndiye mtendaji wa chama hicho kwenye wilaya hiyo. Alisema
yeye ndiye mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho hivyo hatakubali kuona
viongozi wa CCM waliopo madarakani wanafanyiwa fitina na wanachama wa
chama hicho kabla ya muda kufika.
Alisema
mbunge wa jimbo hilo ni James Ole Millya hadi mwaka 2020 hivyo
wanaohitaji kugombea nafasi hiyo wasubiri hadi kipindi hicho kwani
wanaojipitisha hivi sasa watakuwa wanafanya makosa. "Wanachama wa CCM
mnapaswa kuanza kufanya fitina na kupitapita kwenye kata, vijiji au
vitongoji vinavyoongozwa na viongozi wanaotokana na CCM," alisema
Kidunda.
Alisema
hata nafasi za udiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wanaotokana
na CCM wanapaswa kuachwa wamalize nafasi zao na siyo baadhi ya wanachama
kuanza kampeni mapema. Mmoja kati ya wanachama waliojiunga na CCM
Raphael Mollel alisema ubabaishaji uliokuwa CCM awali ndiyo uliwakimbiza
Chadema ndiyo sababu wamerejea CCM.
"CCM
ya Simanjiro ilikuwa inakata majina ya watu na kuendeshwa kindugu
tukahama ila sasa tumerudi kwenye chama chetu kumfuata mbunge wetu
Millya ambaye tulikuwa naye Chadema," alisema Mollel.
BY RICH VOICE
No comments:
Post a Comment