Friday, March 13, 2015

AJALI MBAYA YA BASI LA ABIRIA NA LORI LA MIZIGO JIJI ARUSHA

Tukiendelea kukumbuka tamko la Unabii kutoka kwa Nabii Mkuu Dkt. GeorDavie kuhusu majanga mbalimbali nchini,takribani watu watano wamejeruhiwa ,
katika ajali iliyohusisha magari mawili ikiwemo lori la Mizigo  Semitrela na basi la abiria likitokea Arusha kuelekea Dodoma .
Ajali hiyo imetokea leo  asubuhi katika eneo la Kisongo uwanja wa ndege(Arusha Air Port)  ambapo ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Arusha Express lenye namba T 206 BEF na lori la mizigo kampuni Crewary lenye namba T 493 AED.

Kwa mujibu wa majeruhi  na shuhuda watukio hilo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi lilokuwa likitokea Arusha kuelekea Dodoma alipotaka kupita gari lingine lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na hamadi alikutana na lori la mizigo lililokuwa linatokea Manyara. 
Kufutia ajali hiyo baadhi ya wakazi wa jiji la arusha wamelitaka jeshi la polisi kufanya ukaguzi mara kwa mara ili kubaini baadhi ya watu wanaondesha vyombo vya usafiri wakati huo wakiwa hawana sifa za kuendesha magari.
Kwa upande  Bwana Miraji Ally mkazi wa Arusha amesema kumeibuka wimbi la madereva wanaondesha magari hasa ya abiria wakati huo wakiwa wanafanya mashindano wao kwa wao hali inayosababisha  kutokea ajalia ambazo zimekuwa zikigharibu maisha ya watu kila siku.
Aidha kamanda wa jeshi la Polis Mkoa Wa Arusha  Leberatus Sabasi amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea kufanyika  huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Mkoa Maunt Meru.





No comments:

Post a Comment