Thursday, March 26, 2015

IBADA YA CHUO CHA UPONYAJI TAREHE 26/MARCH/2015

Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr.Geordavie ametangaza siku 14 za kufanyika kwa mambo makubwa maishani kwawalewote wanaomuamini nabii kuanza mwao
Maelfu ya watu wamekusanyika katika chuo kikuu cha manabii Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha katika ibada ya chuo cha uponyaji,ambapo wamefunguliwa vifungo mbalimbali na kupokea maneno ya kinabii ya kuwavusha katika maeneo mbalimbali.Katika ibada hiyo Nabii Mkuu amesema kuwa Mungu anafanya mambo makubwa kwa watu wake.

Huku akiendelea kufundisha juu ya Mamlaka na Utukufu na kufafanua kuwa utukufu ni Fahari na Uzuri, na ya kwamba mahali popote penye fahari na uzuri watu lazima wanakuwa wamoja katika kila jambo,hivyo kama mahali hakuna utukufu umoja hauwezi kuwepo.
Watumishi Wahuduma ya Ngurumo Ya upako Pamoja na Watumishi kutoka katika Huduma zingine wakipokea Baraka
za Kinabii kutoka kwa Nabii Mkuu Mhe.Dkt. GeorDavie .

Aliendelea kueleza kuwa kuna tofauti kati ya Nguvu ya mamlaka na  Mamlaka ya nguvu ya  kwamba watu wengi pamoja na watumishi wa Mungu hivi leo hawana nguvu ya mamlaka ndani yao Bali wana mamlaka ya nguvuKadhalika katika ibada hiyo Nabii Mkuu ametangaza siku 14 kwa watuu wanaomuamini nabii kuanza kuona mambo makubwa yakitendeka maishani mwao na kuendelea kusema kuwa katika siku hizi 14 ni siku za kula faida.


SIKILIZA NA KUDOWN LOAD NENO LA BARAKA ZA SIKU 14  ZA KULA FAIDA.


No comments:

Post a Comment