Monday, March 23, 2015

AJALI MBAYA YA BASI ASUBUHI YA LEO JIJI ARUSHA

Takribani watu 18 wamenusurika kufa leo baada ya gari la abiria lenye T 349 C XB Kampuni ya
Sharoni liliokuwa linatikea Arusha kulekea Singida kuanguka katia eneo la kisongo uwanja wa Ndege Jijini Arusha.
 Kwa mujibu wa abiria walikuwa ndani ya basi hilo wamesema kuwa ali hiyo imetokea baada ya dereva wa basi hilo kutaka kupita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na ndipo gari hilo lilipo acha njia kupinduka.

Kwa upande wa abiria wa basi hilo aliteyejitambulisha kwa moja la Mama Latifa amesema gari hilo lilipoteza muelekeo kuwa mara baada ya gari hilo kufeli breki za nyuma.

Aidha majeruhi watukio hilo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa Maunt Meru Jijini Arusha na wengine wameendelea na safari huku jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo iliotokea majira ya saa moja na nusu leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment