Thursday, March 5, 2015

IDADI YA WALIO KUFA NA MAFURIKO SHINYANGA YAONGEZEKA NA KUFIKIA 42.





Idadi ya watu waliokufa kutokana na mvua kubwa na mafuriko wilayani Kahama, mkoani Shinyanga sasa imefikia 42. Watu wengine 98 wamejeruhiwa, nyumba 160 zimebomolewa na jumla ya watu 570 wameathirika na mafuriko hayo. Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga, amesema
Utawala wa mkoa wake kwa sasa unakusanya michango kwa ajili ya kuwapataa watu hao msaada wa chakula, vyombo na mavazi. Wale waliokosa makazi wamepata hifadhi kwa ndugu na marafiki na pia katika majengo tofauti, likiwemo jengo moja la shule na jengo la mfanyabiashara mmoja wa Kahama. Aidha hapo jana Rais Jakaya Kiwete ameelezea huzuni yake akisema ameshtushwa na maafa hayo huku akisema kuwa maafa hayo si ya wanashinyanga tu bali ni ya watanzania wote.


No comments:

Post a Comment