Monday, November 13, 2023

NABII MKUU" ACHA KULIPIZA KISASI SAMEHE UISHI KWA AMANI NA FURAHA."

Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie Balozi wa Amani amewataka watu kuacha tabia ya kulipiza kisasi kwa watu waliowakosea na badala yake wawe watu wa kusamehe ili waweze kupokea Baraka zao kutoka kwa Mungu.


Nabii Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akifundisha somo lililokuwa na kichwa kisemacho "Kumjua Mtakatifu ni Ufahamu"i katika ibada ya chuo kikuu cha manabii ambapo ilikuwa ni ibada ya kuongozeka kiuchumi.

Akizungumza Nabii Mkuu amesema kuwa makosa ni mengi hivyo kinachotakiwa ni kuishi katika ufahamu huku akieleza jinsi ambavyo yeye amedumu kuwasamehe watu wengi ambao walimkosea maishani.

Na Beatrice Maina, N Y.U ARUSHA.


No comments:

Post a Comment