Friday, November 17, 2023

NABII MKUU KUPOKEA ZAWADI ZA PONGEZI JUMAPILI HII NOV 19, 2023

Nabii Mkuu Mheshimiwa Dkt.GeorDavie anatarajia kupokea zawadi za pongezi kwa kuanzisha Ngurumo ya Upako  Radio ( N.Y.U. FM 99.3 MHz) kutoka kwa watoto wake wa kiroho.

Nabii Mkuu atapokea pongezi hizo ambazo ni kwa mfumo ya fedha katika ibada ya chuo kikuu cha manabii itakayofanyika jumapili katika nyumba ya matamko Ngurumo ya Upako Kisongo jijini Arusha ambapo itakuwa ni ibada ya kupanda viwango kimaisha.

Akizungumza kuhusu Radio Kadinali wa kwanza wa huduma ya Ngurumo ya Upako Mtume Gaudensia Luila amesema kuwa siku tutamshukuru Mungu kwa ajili ya radio ambayo imefanyika Baraka na msaada mkubwa kwa watu wengi ambapo kupitia radio watu wamepomea uponyaji, mitaji na Baraka mbalimbali za kiroho na kimwili.

Amesema tunapomshukuru Mungu kwa ajili ya radio pia ni wajibu wetu kumpongeza Nabii Mkuu ambaye ndiye muanzilishi na msimamizi wa Radio.

Aidha katika ibada hiyo kila mtu atapata nafasi ya kusapoti Radio pamoja na kumpongeza Nabii Mkuu kwa mambo mengi anayoyafanya kwa watu bila mbalimbali kubagua na huduma kwa ujumla.

Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA. 



No comments:

Post a Comment