Wednesday, September 6, 2017

MAFUTA YA TAA YASHUKA, PETROL, DIZELI BEI JUU.

Mamlaka  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya ya bidhaa za mafuta ya petroli nchini, ambapo kuanzia leo bei za rejareja za bidhaa hizo zimepanda kwa Sh 10 kwa lita, ikilinganishwa na bei iliyopita huku bei ya mafuta ya taa ikishuka.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Godwin Samwel, kuanzia Septemba mwaka huu, bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka

ACACIA YAANZA KUFUNGASHA VIRAGO YAKABIDHI UWANJA WA NDEGE WA BUZWAGI.

Baada ya Acacia kutangaza kupunguza operesheni zake Bulyanhulu, kampuni hiyo imeanza kuikabidhi Serikali baadhi ya mali zake kwenye Mgodi wa Buzwagi ambao unatarajiwa kufungwa miaka mitatu ijayo.
Katika utekelezaji wa makabidhiano hayo, jana kampuni hiyo iliikabidhi Serikali uwanja wa ndege uliopo katika mgodi huo. Huu ni mgodi wa pili kufungwa na kampuni hiyo baada ya ule wa Tulawaka ambao iliuuza kwa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) mwaka 2013.
Jana, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Zainab Telack alisema hiyo ni hatua ya awali katika mchakato wa mgodi huo kusitisha shughuli zake za uchimbaji madini kwa mujibu wa mkataba uliopo.
“Tumeanza na uwanja wa ndege baadaye tutakabidhiwa majengo na vitu vingine kama ulivyo utaratibu,” alisema Telack.
Alisema Desemba mwaka huu utakuwa mwisho wa shughuli za uchimbaji na

WATU WAFANYA MAANDALIZI YA MWISHO KABLA KUWASILI KIMBUNGA IRMA.

Visiwa vilivyo eneo la Caribbean vimefanya matayarisho ya mwisho kwa kimbunga Irma, ambacho ni kimbunga chenye nguvu zaidi kwa mwongo mmoja, huku maafisa wakionya kuwa kimbunga hicho kinaweza kuwa chenye madhara makubwa.
Hurrican Irma on 5 September
Kimbunga Irma

Tuesday, September 5, 2017

WATOTO WALIOTEKWA WAKUTWA WAMEKUFA CHOONI

Watoto 2 Ikram na Maureen, kati 4 waliotekwa wamepatikana wakiwa wamefariki dunia katika shimo la choo ambacho  bado halijaanza kutumika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian Olasiti jijini Arusha, Daudi Safari, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi la Polisi limeopoa miili ya watoto hao  jana jioni.
Inadaiwa kuwa mtekaji aliwatumbukiza ndani ya shimo hilo wakiwa hai kabla ya

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO, Jumatano,September06,2017.


HII NDIVYO ILIVYOKUWA KWENYE IBADA YA CHUO CHA MANABII SIKU YA JUMANNE YA TAREHE 05/09/2017

 MCHUNGAJI WA WATOTO  MWANAFUNI HAPPY ALLAN AKIHUBIRI IBADANI HAPO
 MCHUNGAJI  ANNA PETER SALAJE AKIHUBIRI SIKU YA LEO JUMANNE NA HAPA NCHINI NI BAADHI YA WATU WALIOFIKA IBADANI HAPO WAKIHUDUMIWA

ASKARI AKAMATWA SAKATA LA UTEKAJI WATOTO

Wakati Mtuhumiwa wa matukio ya utekaji watoto, Samsom Petro (18), ambaye jana alifikishwa Arusha kwa ajili ya kuonyesha sehemu alipowaficha watoto, amebainika kuwa anaishi na kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa.
Inadaiwa kuwa askari huyo pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano tangu Agosti 27 wakati kikosi maalum cha polisi kilipozingira nyumba aliyopanga.
Petro, ambaye alikamatwa juzi akiwa Katoro mkoani Geita, anatuhumiwa kuwateka watoto wawili, Moureen David(6) na Ikram Salim(3) na hadi jana jioni alikuwa ameandamana na polisi katika eneo la Njiro ambako alidai aliwatelekeza watoto hao.
Lina Kajuna ambaye ni mmiliki wa nyumba ya aliyekuwa amepanga askari huyo wa FFU, alisema ana miaka miwili tangu ampangishe.
Kajuna alisema mtuhumiwa wa utekaji, Samson Petro alifika Arusha mwezi Juni

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO,Jumanne,September05,2017.


Monday, September 4, 2017

UWEKEZAJI MOROGORO WAWAWEKA MATATANI RAIA WATATU WA CHINA

Siku moja baada ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa agizo kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro kufuatilia utendaji wa kampuni ya Zhong Fenq, umeviagiza vyombo vya ulinzi kuwakamata raia watatu wa China wanaodaiwa kuendesha shughuli za uwekezaji kinyume cha sheria.
Image result for kassim majaliwa
Juzi, Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen

WAZIRI KASIM MAJALIWA KESHO KUZINDUA MFUMO WA UANDAAJI BAJETI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Jumanne Septemba 5 atazindua mifumo miwili itakayosaidia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama wakati wa ufuatiliaji na uandaaji wa bajeti nchini.
Katika uzinduzi huo, mawaziri sita ambao wanafanya kazi na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) watahudhuria.
Kiongozi wa timu ya rasilimali fedha, Dk Gemini Mtei amesema uzinduzi huo