Wednesday, August 16, 2017

HATUA ZA KUFUATA ILI KUYAFIKIA MAFANIKIO.



Uvumilivu, hekima na kulishika neno la mungu maishani ni moja ya hatua zitakazomfanya mwanamke kuyafikia malengo aliyojiwekea.

Hayo yamesemwa na wamama wakati wakizungumza katika kipindi cha wamama na majukumu kinachorushwa na N.Y.U Radio kilichokuwa na mada inayosema njia zinazotumika kutimiza malengo.
 

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA.

Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa Tottenham Danny Rose, 27, baada ya mchezaji huyo kushutumu sera za usajili za Spurs. (Sun)

Tottenham wamefikia makubaliano na PSG kumsajili beki Serge Aurier, 24, ambaye alikuwa akifuatiliwa na Manchester United. (L'Equipe)

Tottenham wana uhakika wa kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Ajax, Davinson Sanchez, 21, kwa pauni milioni 27. (Daily Mirror)

SOKO KUU SIDO JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO.



Soko kuu la Jijini Mbeya maarufu kama SIDO limeungua moto usiku wa kuamkia leo .Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku ambapo mali za wafanyabiashara mbalimbali katika soko hilo zimeteketea.

JAPANI YAKUBALI KUMALIZA FOLENI DAR. .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 15 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Mbunge na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Ichiro Aisawa Ikulu Jijini Dar es Salaam.


HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO. Jumatano,August 16,2017.


Tuesday, August 15, 2017

WATU 27 WAUAWA NIGERIA.



Mtu aliyejitoa mhanga ameua takriban watu 27 kaskazini mashariki mwa Nigeria na kujeruhi wengine zaidi ya wanane.
Vyombo vya usalama katika eneo hilo vimesema, watu watatu waliojitoa mhanga akiwemo mwanamke mmoja, walijilipuwa wenyewe kwenye lango la kuingilia kambi ya wakimbizi.

DKT. KALEMANI AENDELEA KUZINDUA MIRADI YA UMEMEMVIJIJINI AWAMU YA TATU (REA PHASE III MIKOA YA KUSINI NA RUKWA

                                                                                           
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani ameendelea na ziara za uzinduzi wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA PHASE III) ambapo Agosti 14, 2017 alikuwa Mikoani Rukwa katika Kijiji cha Kabwe Wilaya ya Nkasi.Dkt. Kalemani alisema jumla ya Shilingi Bilioni 42.5 zitatumika kupeleka umeme katika Mkoa huo na kuongeza Mradi huo utatekelezwa katika vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 111.

Uhuru Kenyata Aruhusu Maandamano ya Wakenya Wanaompinga na Amewataka Polisi Wawape Ulinzi


Rais Uhuru Kenyatta huenda akaingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia kwa marais wa Afrika kwa kuamua kuruhusu maandamano ya amani kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.




Waziri Mkuu Awabana Maafisa Ushirika, Kilimo........Ataka wasimamie zao la tumbaku kwa umakini ili kumkoboa mkulima

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maafisa kilimo na maafisa ushirika wa mkoa wa Tabora wasimamie kwa umakini ukuzaji wa zao la tumbaku kuanzia msimu ujao.


Mambo 10 Ambayo Tanzania na Misri Zimekubaliana Kushirikiana baada Ya Rais Wao Kutua Nchini Jana



Tanzania  na Misri zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika maeneo makuu 10, ikiwemo kuimarisha uhusiano, ulinzi na kujenga kiwanda kikubwa cha nyama pamoja na kiwanda cha dawa nchini.
Pamoja na makubaliano hayo ya kiuchumi na kijamii, suala la matumizi ya maji ya Mto Nile halijapatiwa muafaka na mazungumzo yanaendelea kuwezesha kukamilisha matumizi yenye faida ya mto huo kwa nchi zote zinazohusika.

DODOMA SASA KUJENGWA UWANJA MPYA WA TAIFA.

Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Dodoma ilitenga Ekari 143 zilizopo Nara Barabara ya Singida nje kidogo ya mji wa Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na kituo cha michezo kitakachojengwa kwa msaada wa serikali ya Morocco.




ZUMA ASEMA WATU WALIPANGWA KUNIUA

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini wikendi iliopita alizungumzia kuhusu jaribio la kumuua akisema kuwa aliwekewa sumu na karibu afariki kutokana na msimamo wake wa kiuchumi na marekebisho ya umiliki wa ardhi.