Marekani imeyataka
mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na
Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la
masafa marefu.
Kocha wa Manchester City, Pep
Guardiola, amesema kujiamini kwa Raheem Sterling kumemfanya awe na
kiwango bora baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Southampton
katika dakika ya 96.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger,
amempongeza mpambanaji Mesut Ozil baada ya raia huyo wa Ujerumani
kuchangia ushindi mnono wa klabu hiyo wa magoli 5-0 dhidi ya
Huddersfield.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro
kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya
Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya
semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.
Korea
Kaskazini imelifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu
lililoruka juu zaidi na kudumu angani kwa dakika 53 kabla ya kutua
katika bahari ya Japani.
Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa taarifa kwa wateja katika mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani kuwa baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na
hitilafu iliyojitokeza.
Kwa
mara ya kwanza, Tundu Lissu amezungumzia shambulio la kinyama
alilofanyiwa na watu wasiojulikana kwa kueleza kuwa, alinusurika
kufumuliwa fuvu la kichwa kwa risasi.
MKUU
wa jeshi la polisi nchini (IGP)Simon Sirro amewahakikishia wananchi
mkoani Pwani kuwa silaha zote zilizochukuliwa na wahalifu wa ovyo ovyo
huko Kibiti na Mkuranga zimerudi zote mkononi mwa dola na kusambaratisha
mtandao wa kiuhalifu .
Picha za wavulana
wawili wa Kichina ambao walisafiri na basi moja kwa umbali wa kilomita
80 wakiwa chini ya gari hilo zilizua hisia kali kuhusu hali ya watoto wa
taifa hilo waliowachwa nyuma.