Tuesday, March 6, 2018

MAN UTD YACHOMOA MAGOLI MAWILI NA KUIBUKA NA USHINDI

Nemanja Matic amefunga goli tamu la dakika ya mwisho na kuipatia ushindi Manchester United iliyokuwa nyuma kwa magoli 2-0 na kukwea hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi.

Mkapa amteua Prof. Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) Kuchukua Nafasi ya Profesa Kikula

Na Paschal Dotto-MAELEZO    
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe. Benjamin William Mkapa ametangaza uteuzi wa  Profesa Egid Beatus Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Idris Suleiman Kikula.

Freeman Mbowe aruhusiwa kutoka hospitali. Daktari aeleza ugonjwa wake

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) ameruhusiwa kutoka hospitali hapo baada ya madaktari kujiridhisha kuwa afya yake imeimarika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 6

Rais Magufuli atoa kibali cha kuendelezwa ujenzi wa msikiti wa Sumbawanga......Serikali ya mkoa wa Rukwa yachangia Milioni 5.7 kuumalizia

Uongozi wa Waislamu Mkoani Rukwa umepokea kwa furaha mchango wa Shilingi Milioni 5.7 uliotolewa na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika kikao cha maridhiano juu ya ujenzi wa msikiti uliosimama kwa muda.

Ufaransa Yaipongeza Tanzania Kwa Kupambana Na Rushwa

SERIKALI ya Ufaransa imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mapambano dhidi ya rushwa na inaamini fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali zitatumika kama ilivyokusudiwa.

Friday, February 16, 2018

Trump lawamani na sheria ya silaha

Shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouwawa 

Chama cha Democrats kimewashutumu Rais Donald Trump na Spika wa bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha.

Hiki ndicho kituo cha kazi alichopangiwa Balozi Dkt Slaa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Februari, 2018 saa 3:00 asubuhi atawaapisha Mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.

WENGER AIPONGEZA ARSENAL BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI SWEDENI

Arsene Wenger amekipongeza kikosi chake cha Arsenal kwa namna walivyomudu mazingira mageni na kuifunga Ostersunds FK ya Swedeni kwa magoli 3-0 katika mchezo wa Ligi ya Europa

Watanzania wawili wakamatwa China wakiwa na kete 129 za dawa za kulevya

Watanzania wawili, Baraka Malali na mkewe Ashura Musa wamekamatwa nchini China wakiwa wamemeza

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya February 16

Thursday, February 15, 2018

Afrika Kusini: Ramaphosa kuapishwa kuwa rais

Cyril Ramaphosa 
Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa Afrika Kusini baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu.