Wednesday, February 5, 2014

(HABARI). Erdogan aiomba Ujerumani isaidie

      Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan  ameiomba Ujerumani iiunge mkono nchi yake katika juhudi za nchi hiyo za kuwania kujiunga na
Umoja wa Ulaya.Waziri Mkuu wa Uturuki aliefanya ziara fupi nchini Ujerumani na kukutana na Kansela Angela Merkel amesema kuwa Ujerumani kwa sasa haiiungi mkono nchi yake kwa kiwango cha kutosha katika suala la kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo kwa upande wake Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema kuwa anayaunga mkono mazungumzo juu ya Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya lakini anayo mashaka iwapo Uturuki ijiunge   na Umoja huo. Ujerumani na Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya hivi karibuni zilionyesha wasi wasi juu ya hali ya demokrasia nchini Uturuki katika muktadha wa hatua zilizochukuliwa na polisi ili kuwakabili waandamanaji. Ujerumani na Umoja wa Ulaya pia zina mashaka juu  ya hatua zinazochukuliwa na Uturuki katika kuleta mageuzi katika mfumo wa sheria.
           

No comments:

Post a Comment