(NEWS). UJERUMANI WAKIRI KUONGEZA UIMARA WA KIJASUSI DHIDI YA NCHI ZA MAGHARIBI.
Hayo ni kwa
mujibu wa ripoti ya jarida la kila wiki la Ujerumani, Der Spiegel.Ripoti hiyo
inasema balozi za nchi za magharibi kama vile Marekani na Uingereza hapa
Ujerumani zitafuatiliwa kwa karibu zaidi.
Kwa sasa
Ujerumani huzifuatilia kwa karibu nchi kama vile Urusi na China, lakini
haizilengi nchi zilizo washirika wake kwa kiwango kama hicho.
Inafikiriwa
kwamba simu ya kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ilifuatiliwa kutoka ubalozi
wa Marekani mjini Berlin.
Jarida la
Spiegel linasema mipango hiyo inafuatia ufichuzi wa udukuzi wa kiwango kikubwa
uliofanywa na shirika la usalama wa kitaifa la Marekani, NSA.
No comments:
Post a Comment