alikamatwa. Msemaji wa Polisi mjini Geneva Christophe Fortis, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba, ndege hiyo aina ya ET-702 iliotoka Addis Ababa kuelekea Roma ilitekwa na kutua mjini Geneva saa kumi na mbili asubuhi. Msemaji huyo wa polisi amesema uwanja wa ndege kwa sasa umefungwa na hali imedhibitiwa. Kulingana na polisi wa uwanja wa ndege mjini Geneva ,aliyeiteka nyara ndege hiyo ni rubani msaidizi aliepata nafasi hiyo baada ya rubani mwenzake kwenda msalani. Rubani huyo msaidizi aliye na umri wa miaka 31, amesema anahofia maisha yake nchini Mwake na anataka kuomba hifadhi nchini Uswisi.
Ndege hiyo aina ya Boeing 767 iliondoka Addis Ababa saa sita na nusu usiku saa za Addis Ababa na ilitarajiwa kutua katika mji mkuu wa Italia Roma saa kumi na dakika arobaini leo asubuhi.
Tazama Video hapa chini..
. ...........hisani ya DWSWAHILI...................
No comments:
Post a Comment