Rais wa Ukraine akubali kufikia makubaliano na upinzani
Rais wa Ukraine Viktor Yanukovich ametangaza
makubaliano na viongozi wa upinzani na kuanza
majadiliano kumaliza umwagikaji wa damu. Taarifa hiyo
imekuja baada ya mkutano pamoja na viongozi watatu
wa upinzani, Vitali Klitschko, Arseny Yatseniuk na
mwanasiasa mwenye mtazamo wa kizalendo anayefuata
siasa kali za mrengo wa kulia Oleh Tyahnibok. Wakati
huo huo rais wa Marekani Barack Obama ametuma
ujumbe kwa serikali ya Ukraine kushughulikia ghasia
zinazotokea nchini humo za kuipinga serikali kwa njia
ya haki.Watu 26 wameuwawa katika ghasia za mitaani mjini
Kiev tangu Jumanne. Tovuti ya rais imetangaza kuwa
polisi hawatavamia makambi ya waandamanaji katika
uwanja wa Uhuru kama ilivyopangwa . Katika hatua
nyingine jana jioni, rais alimbadilisha mkuu wa jeshi la
Ukraine. Katika mkutano wa pamoja na waandishi
habari mjini Paris jana Jumatano kansela wa Ujerumani
Angela Merkel na rais wa Ufaransa Francois Hollande
wametoa wito wa kuwekwa vikwazo maalum dhidi ya
uongozi wa Ukraine. Waziri wa mambo ya kigeni wa
Ujerumani Frank-Walter Steinmeier atajiunga na
wenzake wa Ufaransa na Poland mjini Kiev leo Alhamis.
No comments:
Post a Comment