Wednesday, March 26, 2014

EXCLUSIVE NEWS -Muasisi wa manabii Tanzania mh Dr GeorDavie awahudumia watu kwa njia ya mtandao wa Facebook.


Ikiwa ni siku 3 tangu Muasisi wa manabii Tanzania mh Dr GeorDavie aitangaze wiki hii kuwa ni wiki ya kutembea katika neno moja tu la kinabii, mapema leo saa nne asubuhi, amewahudumia watu kwa njia ya mtandao wa kijamii Facebook.

Nabii mkuu amewahudumia watu mbalimbali wenye matatizo ikiwa ni pamoja na kuwatamkia maneno ya kinabii yenye kuwajenga, kuwatia moyo, kufufua na kuwarudishia matumaini tena walio kata tama maishani mwao.Huduma hiyo ya pekee iliyodumu kwa takriban dakika 45, nabii alilenga kuwasikiliza watu kupitia mtandao huo wa kijamii huku akijibu mahitaji ya yeyote aliyehitaji neon la kinabii.Wakitoa maoni yao baadhi ya watu kuhusiana na dakika hizo za Baraka wamemshukuru nabii mkuu kwa kudumu kuwahudumia wakati wote.Sekela Ntondolo, ambaye ni mtume na balozi wa nabii mkuu Nchini Marekani ameitaja nafasi hiyo kuwa ni yapekee huku akimpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya anajisikia furaha kuwa binti yake, kwani amepata upenyo na ushindi maishani siku zote.
Akihitimisha huduma hiyo nabii mkuu amewatamkia watu wote kupokea ushindi katika kila hitaji, na kubofya kitufe cha ‘’LIKE’’ kama ishara ya kupoke mahitaji yao, hata sasa unaweza kufanya hivyo.





  1. NINA DAKIKA 45 ZA KUWA KWENYE MTANDAO KUKUSIKILIZA .. — feelinghappy.
    Like ·  · 

No comments:

Post a Comment