Sunday, March 9, 2014

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 09-03-2014


Ilikuwa juamapili ya baraka na yenye nguvu na Muujiza kwa maelfu ya waumini wa Ngurumo ya Upako walio kusanyika katika Hema la kukutania Kisongo Arusha,
wakati ambao maelfu ya waumini hao walirekebishiwa maisha na Kufunguliwa kutoka katika utumwa wa Nguvu za Giza na kuwa wanawapya ndani ya Yesu.
 Ambapo kiongozi Mkuu wa Huduma Ya Ngurumo Ya Upako Duniani na Nabii Mkuu Dr. GeorDavie ambapo aliwatamkia maelfu ya waumini neno la kinabii kuwa hii ni wiki ya KUENDELEA KUREKEBISHIWA MAMBO YAKO. Hata hivyokulikuwa na watu walio kuja toka sehemu mbalimbali na kutoa shuhuda zao ambao Mungu wa GeorDavie kawatendea katika Madhabahu itowayo Moto na Ngurumo.



 Sanjari na mafundisho hayo lakini pia Nabii mkuu Dr.GeorDavie aliweza kumpa nafasi Nabii kutoka Africa ya Kusini Nabii Harry Kgmothoso aliyekuwa katika mafunzo ndani ya chuo cha Manabii cha Ngurumo ya Upako,ambapo Nabii Kgmothoso aliweza kueleza juu ya Nguvu ya Mungu aliyo kutana nayo ndani ya Huduma ya Ngurumo Ya Upako pia Alieleza jinsi Nabii mkuu wa Karne ya 21 alivyo Mnyenyekevu Mbele za Mungu licha ya kuwa mtu Mashuhuri Duniani kutokana na kazi kubwa ya huduma anayoifanya.




Mwimbaji wa nyimbo  za Injili MICHAEL PETRO akiimba mara baada ya kupewa nafasi ya kuimba na Nabii mkuu Dr. GeorDavie

SIKILIZA NA KUDOWNLOAD NENO LA KINABII LA WIKI HII HAPA CHINI.

No comments:

Post a Comment