Friday, January 25, 2019

VITUO VYA WATOTO YATIMA VYAPOKEA MSAADA WA CHAKULA.




    Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa misaada ya vyakula vyenye thamani ya sh. 3,120,000 (milioni tatu laki moja na elfu ishirini) kwa vituo viwili vya watoto yatima siku ya leo.
   Misaada hiyo imekabidhiwa asubuhi ya leo kwa niaba ya Nabii Mkuu nae Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila kwa wasimamizi wa vituo vya Faraja Orphanage center, Bw. Faraja, pamoja na kwa msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care anayeitwa Mchungaji Zakia Hatib.
   Vitu vilivyotolewa ni pamoja na mchele kg. 600 wenye thamani ya sh. 1,320,000 (milioni moja, laki tatu na elfu ishirini), mafuta ya kupikia lita 300 yenye thamani ya sh. 1,200,000 (milioni moja na laki mbili) pamoja na sukari kg. 240 yenye thamani ya sh. 600,000 (laki sita).
   Wakizungumza baada ya kupokea misaada, wasimamizi wa vituo hivyo wametoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kwa upendo wake pamoja na moyo wa kusaidia alionao kwa watu wote bila kujali dhehebu, dini wala kabila.
   Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali katika vituo vya watoto yatima kila mwanzo wa mwaka ambapo zoezi hilo litaendelea kwa vituo vingine.

NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio




Pichani ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) akikabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie,  kwa msimamizi wa kituo cha Faraja Orphanage.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa kama misaada katika vituo vya watoto yatıma.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa katika  vituo vya watoto yatima.

Baadhi ya vyakula vilivyotolewa kwa watoto yatima.

Katika picha ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) katika picha ya pamoja na Msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care, wakati akimkabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.

Tuesday, January 22, 2019

ATOA ZAWADI YA PIKIPIKI NA PESA KEM KEM KAMA ZAWADI KWA WATU WALIOWEZA KUJIBU MASWALI!


Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amezidi kubariki jamii kwa kumwaga pesa ikiwa ni mara baada ya kutoa zawadi ya pikipiki pamoja na pesa taslim, zaidi ya shilingi milioni moja kama zawadi.

Nabii Mkuu alitoa zawadi ya Pikipiki yenye thamani ya shilingi Milioni mbili na laki nne (2,400,000) kwa Ndugu. Tito Paul pamoja na zawadi ya pesa alizojishindia kwa kujibu maswali aliyomuuliza kwa ufasaha kabisa.
Kwa upande wake Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie akizungumzia hilo amewataka watu kuchangamkia nafasi ya kujibu maswali hayo kwani kwa kufanya hivyo watajiongezea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kama magari, nyumba, pikipiki na pesa za mtaji, ada na za kujikimu katika mahitaji mengine.
Akielezea mgawanyiko wa maswali yanayoulizwa katika vipindi hivyo Nabii Mkuu amesema kuwa maswali hayo yamegawanyika katika sehemu tatu (3).. 60% yakiwa yanahusu huduma, 20% N.Y.U Radio na 20% nyingine yakiwa yanahusu GeorDavie Tv ambapo watu wametakiwa kufuatilia vipindi kwa makini pamoja na kuhudhuria ibada katika Hema la Kukutania Ngurumo Ya Upako ili kupata uelewa zaidi wa kuweza kujieleza ili waweze kushinda zawadi hizo.
Akifafanua zaidi Nabii Mkuu amesema kuwa haya ni majira mapya ambayo Serikali Tukufu Ya Ufalme Wa Mungu inawabariki watu wake kwa njia ya tofauti ambapo amesema kuwa zoezi hilo bado linaendelea.
Tangu kuanza kwa mwaka huu Nabii Mkuu ametoa zaidi ya shilingi milioni nane (8) kwa jamii, ambapo zawadi hizo watu wamekuwa wakijishindia kwa njia ya kujibu maswali katika vipindi mbalimbali vinavyoruka kupitia 99.3 N.Y.U RADIO pamoja na GEORDAVIE TV.
Katika muendelezo wa utoaji wa zawadi hizo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwepo tena katika kipindi cha "Q & A AKILI KUBWA" kitakachoruka Live kwa njia ya 99.3 N.Y.U RADIO pamoja na GEORDAVIE TV jumatano ya week hii, kuanzia majira ya saa mbili na nusu usiku, ambapo atakuwa akiuliza maswali na kutoa zawadi ya pesa kwa washindi watakaojibu vizuri.
Aidha Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ameitangaza week hii kuwa ni week ya kung'oa kila pando la adui na mabaya yote na kuongeza kuwa week hii Roho Wa Mungu atadumu kung'oa kila pando la adui lenye lengo la kudhoofisha watu.
NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Tuesday, January 15, 2019

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE ATANGAZA WIKI YA USHINDI KATIKA MAENEO YOTE MAISHANI.




 KUTOKA IKULU YA NABII MKUU TANZANIA..

    Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwa hii ni wiki ya kuwa washindi katika maeneo yote maishani.
    Ameyasema hayo wakati akiongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania, Ngurumo Ya Upako, Kisongo, Arusha.
   Katika ibada hiyo ambayo pia ilikuwa ni ibada ya Silver Partners, Nabii Mkuu alitamka baraka mbalimbali za Kinabii kwa wana-Partners wote ikiwemo baraka ya kushika pesa na kuheshimika.
   Aidha Nabii Mkuu alifundisha umuhimu wa kuwa mwana-Partners na faida zake huku akiwasisitizia watu wote kusapoti kazi ya Mungu kwa nguvu kwa kuna baraka ya kipekee wataipata kwa kufanya hivyo na kuwakumbusha kuwa ili kazi ya Mungu iwe nzuri na ithaminiwe ni lazima igharamikiwe ambapo alitoa nukuu isemayo "Cha gharama kina thamani kama hakina gharama hakina thamani" akimaanisha kuwa kitu chochote chenye thamani lazima kiwe cha gharama hakiwezi kuwa bure ikiwemo Nguvu Ya Mungu.
   Wakati huohuo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwepo katika kipindi cha Maswali Na Majibu  kitakachoruka LIVE kwa njia ya Radio,  99.3  N.Y.U FM pamoja na GEORDAVIE TV siku ya jumatano ambapo kwa siku hiyo yeye ndiye atakayeuliza maswali kwa wasikilizaji na watazamaji na kisha kutoa zawadi ya pesa taslimu kwa wale watakaopatia kwa kujibu maswali hayo vizuri. 


          NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Tuesday, January 8, 2019

JE UNAFAHAMU KUWA MHE. DR. GEORDAVIE KATIKA MWAKA 2018 PEKEE AMETUMIA ZAIDI YA SH. MILIONI 143 KATIKA KUSAIDIA JAMII???


   Amekuwa akitambulika kama Mtumishi wa Mungu mtoaji zaidi Nabii wa Equator, Nabii Mkuu wa karne ya 21, si mwingine ni Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie kutoka Arusha, Tanzania.
  Na siku ya leo tunakuletea kwa uchache baadhi ya matukio ya utoaji aliyoweza kuyafanya kwa mwaka wa 2018 yaliyopelekea Nabii Mkuu ambaye amekuwa msaada na kipenzi cha wengi kutajwa kama Mtumishi Wa Mungu mtoaji zaidi.
  Katika ku-support Watumishi Wa Mungu kutoka katika makanisa mengine tofauti na Ngurumo Ya Upako yaliyo ndani na nje ya Tanzania, Nabii Mkuu ametumia zaidi ya Sh. Milioni 30 katika kuhakikisha anatoa misaada katika huduma hizo ambapo kwa asilimia kubwa zilikuwa haziridhishi kiuchumi (hazijamudu kujitegemea kiuchumi), Nabii Mkuu aliweza kuwasaidia ili kuhakikisha watumishi wanaweza kukidhi mahitaji yao lakini pia ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kujenga makanisa yao ili yawe katika hali ya kuridhisha.
  Katika upande mwingine wa kijamii, Nabii Mkuu amekuwa na kawaida ya kupeleka misaada sehemu mbali ikiwa ni pamoja na katika vituo vya watoto yatima ambapo kwa mwaka 2018 Nabii Mkuu amepeleka katika vituo vitatu tofauti hapa Tanzania.
   Mbali na hayo pia Nabii Mkuu ametoa misaada mingine ikiwemo kuwalipia ada wanafunzi wa ngazi mbalimbali mpaka chuo kikuu waliokwama kutokana na kukosekana kwa kipato ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao.
  Aidha katika kusaidia watu pia Nabii Mkuu ametumia zaidi ya Milioni 20 katika kusaidia watu mbalimbali wenye mahitaji, ikiwemo wenye uhitaji wa mitaji lakini pia wenye biashara ndogo ndogo katika kuhakikisha wanaweza kuwa na kipato cha kujikimu kimaisha.
  Lakini pia katika upande mwingine Nabii Mkuu amekuwa akiwa-support watu wenye vipaji kwa namna mbalimbali ambapo baadhi ya waliopata neema hiyo ni pamoja na vijana wawili walionunuliwa ngoma na mwingine spika ,kila mmoja kwa wakati wake pamoja na waimbaji wa nyimbo za injili kutoka sehemu mbalimbali.
  Hakuishia hapo katika kusaidia tu, Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa akitoa zawadi mbalimbali kwa watu ambapo kwa mwaka wa 2018 ametoa zawadi ya magari nane (8) kwa watu tofauti tofauti wa ndani na nje ya nchi kwa mwaka huo yenye thamani ya jumla milioni 88.
  Aidha katika msimu wa sikukuu mpaka sasa Nabii Mkuu ametoa zawadi kwa njia ya pesa taslimu za zaidi ya sh. Milioni 5 kwa watu mbalimbali ambao walijishindia kwa njia ya kupiga simu kwenye vipindi vilivyokuwa vikiruka kupitia 99.3 N.Y.U FM Radio pamoja na GeorDavie Tv (zoezi hilo linaendelea mpaka sasa) na wengine wakijishindia kupitia mitandao ya kijamii.
  Akizungumzia utoaji huo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amesema haya "hiyo ni njia ya Ufalme Wa Mungu kuwabariki watu wake kwakuwa nao wamekuwa wakitoa kwa Ufalme Wa Mungu hivyo sasa ni wakati wao kubarikiwa pia" mwisho wa kunukuu.
         NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.